BASATA YAKUTANA NA WADAU WA SANAA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA KUJENGA MIPANGO YA PAMOJA
Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa, Sensa ya Filamu na Utamaduni kwa upande wa Zanzibar Dkt.Omar Abdalla Adam pamoja na watendaji wake wakutana na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw.Godfrey Mngereza.
Lengo ni kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi hizi mbili kwa kuweka mipango ya pamoja ya utendaji kazi katika mwaka wa fedha 2020/2021.
Lengo ni kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi hizi mbili kwa kuweka mipango ya pamoja ya utendaji kazi katika mwaka wa fedha 2020/2021.
Katika kikao hiki taasisi hizi mbili zimekubaliana kufanya kazi kwa pamoja katika maeneo ya kuwajengea uwezo wasanii na wadau wa sanaa katika suala la mikataba, utoaji tuzo kwa wanafunzi waliofanya vyema katika Mitihani ya kidato cha nne katika masomo ya Muziki, Sanaa za maonyesho na sanaa za ufundi.
Mashirikiano hayo yanalenga kuwaunganisha wasanii na wadau wa sanaa walioko Tanzania Bara na Visiwani.
Kikao hiki kilichofanyika makao makuu ya BASATA jijini Dar Es Salaam ni muendelezo wa vikao vya ushirikiano kati ya BASATA na BASSFU katika kuimarisha ushirikiano wenye tija kwa sekta ya sanaa nchini Tanzania.
No comments: