SERIKALI YAOMBWA KULIINGIZA ZAO LA PILI PILI KICHAA KWENYE MAZAO YA KIMKAKATI.


Mhandishi na mkulima wa Manguajuki manispaa ya Singida,akikagua pilipili kichaa.Bei ya pilipili kichaa kilo ni shilingi 5,000 kwa kilo.
 Sehemu ya ekari tano za shamba la pilipili kichaa la mhandisi/mkulima wa Manguanjuki manspaa ya SingidamHassan Tati.
 Mmoja kati ya miche ya mapapai iliyopo kwenye shamba la pilipili kichaa linalomilikiwa na mhandisi/mkulima Haasan Tati mkazi wa Manguanjuki nje kidogo ya mji wa Singida.
Mhandisi na mkulima na mkazi wa Manguanjuki manispaa ya Singida,akihojiwa na waandishi wa habari juzi juu ya kilimo cha zao la pilipili kichaa.Picha zote na Nathaniel Limu.

 =======  =======  ======  ========

SERIKALI imeombwa kuangalia uwezekano wa kuliingiza zao la pilipili kichaa kwenye mazao ya kimkakati, ili liweze kupewa mkazo zaidi kulimwa kwa madai lina masoko makubwa ndani na nje ya nchi.Na linasadikika lina uwezo mkubwa wa kufumbaza virusi vya Corona vinavyosababisha homa kali ya mapafu.

Akizungumza jana na mwandishi wa habari hii akiwa shambani kwake, mkulima wa kilimo cha umwagiliaji mhandisi Hassan Tati, amesema pia pilipili kichaa ikichanganywa na mazao mbalimbali ikiwemo tangawizi, inatibu saratani ingali changa.

Amesisitiza mhandisi Tati ambaye anajishughulisha na kazi za ukandarasi,kuwa kilimo cha zao hilo, ni rahisi mno na halina changamoto nyingi, ikilinganishwa na mazao mengi ikiwemo nyanya.

“Mche wa pilipili kichaa unazaa vizuri kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo.Baada ya miaka hiyo,unapanda mingine. Kilimo hiki kinaruhusu kupanda miche mingine kama papai na ndizi. Ni kilimo mseto, pilipili kichaa ambazo si bora zikisangwa vizuri, ni dawa bora mno ya kuulia wadudu waharibifu shambani”,amesisitiza zaidi.

Mkulima Tati ametaja faida zingine zitokanazo na pilipili kichaa, kuwa inadaiwa inachanganywa katika maji ya washa washa na mabomu ya machozi yanayotumiwa na jeshi la polisi.

“Chakula cho chote nchini India, lazima kiwe na pili pili hii. Wanatumia kutengenezea dawa na vipodozi mbalimbali. Somalia na Ethiopia, nao vyakula vyao lazima viwe na pilipili tena iwe ya kutosha”,amesema.

Katika hatua nyingine,mkulima huyo amesema kuwa uzuri wa kilimo cha zao la pilipili kichaa,lina wanunuzi ambao hutoa mbegu boora.Katika mbungu hizo,mkulima analipa sehemu ya gharama.

“Kiwango kinachosalia,atakimalizia mara atakapouza mazao yake.Wanunuzi hao wanatoa wataalamu wao kwa ajili ya kueleimisha kilimo bora cha pilipili kichaa.Wanasimia vizuri mwazo hadi mwisho.

Tati ametumia fursa hiyo kuishukuru serikali ya mkoa wa Singida pamoja na halamshauri zake,kwa kutoa wataalam wa kilimo kusimamia na kuwaelemisha wakulima wachache wa pilipili kichaa mkoani ha

Wakati huo huo,mkulima wa zao la pilipili kichaaa wilaya ya Ikungi,Yeremia Yohana amesema kwa vile ndio kwanza wanaanza kilimo hicho,itapendeza zaidi endapo maafisa kilimo na mifugo wilaya ya Ikungi na mkoa,wakawatembelea wakulima mara kwa mara kutoa ushauri na maelekezo. “Nitumie fursa hii kuwakumbusha wakazi wa wilaya ya Ikungi kwamba ugonjwa wa corona upo.Hivyo kila mmoja tuendelee kuchukua tahadhari kwa kujikinga na kudhibiti kusambaa kwa virusi vya Corona.”,amesema Yohana.

No comments: