MKURUGENZI HALMASHAURI YA MWANGA AGAWA VIFAA VYA KUTUNZA MAZINGIRA
Charles James, Michuzi TV
KATIKA kuhakikisha mazingira yanatunzwa pamoja na kuwa safi, Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga imekabidhi vifaa vya utunzaji mazingira kwa timu ya watendaji wake katika bustani iliyopo eneo maarufu la maliasili.
Bustani hiyo imejipatia umaarufu mkubwa wilayani Mwanga ambapo wananchi hufika kupiga picha hasa kwenye matukio muhimu kama Harusi, Mahafali na shughuli zingine.
Vifaa hivyo vimetolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga, Zefrin Lubuva ambapo amesema lengo lao ni kuifanya Wilaya hiyo kuwa ya kijani na inayovutiwa.
Lubuva amesema bustani hiyo imekua kivutio ambapo licha ya wananchi kwenda kupiga picha lakini pia wamekua wakinunua Maua ambayo yanauzwa na vijana walioamua kujiajiri na kufanya kazi kama ambavyo Rais Magufuli anavyosisitiza.
" Nimewakabidhi vifaa hivi vyenye thamani ya Sh Milioni Tano ili muendeleze bustani hii izidi kuvutia na kupendeza. Niwatake pia mzidi kupaboresha na kuongeza ubunifu zaidi.
Vijana wengine wachukue hii kama changamoto kwao, wasikubali kulalamika tu kwamba hakuna ajira wakati wanaeza kuungana kama kikundi wakatengeneza wazo la biashara na kuja halmashauri ili wapewe mikopo wajiendeleze," Amesema Lubuva.
Ameahidi kuendelea kushirikiana na vijana wote wa Wilaya hiyo katika kufanya kazi pamoja na kuwapa mikopo isiyo na riba inayotolewa na halmashauri ili wafanye kazi na kuongeza kipato chao.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga, Zefrin Lubuva (wa pili kushoto) akiwakabidhi vifaa vya kufanyia usafi vijana wanaofanya kazi ya kutengeneza bustani maarufu wilayani hapo pamoja na kufanya usafi.
No comments: