VYAMA VYA SIASA 12 VISIVYO NA WAWAKILISHI BUNGENI VYATANGAZA KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU OKTOBA 25,KUSIMAMISHA WAGOMBEA KILA JIMBO
VYAMA vya siasa nchini visivyokuwa na wawakilishi Bungeni vimetangaza kushiriki katika Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 25 mwaka huu wa 2020 kwa ngazi udiwani na ubunge.
Baadhi ya vyama hivyo ni DP,NRA, AAFP, UMD, UDDP, Makini, TLP,UDP, SAU, NLD, ADC, na CCK ambapo pamoja na mambo mengine vitafanya kampeni katika uchaguzi huo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mratibu wa umoja huo, Rashid Rai amesema wanatangaza kushirikiana katika uchaguzi mkuu kwenye ngazi ya udiwani na ubunge kwa kusimamisha mgombea kwenye kila jimbo”.
Ameongeza kuwa kwa nafasi ya mgombe urais, Rai kila chama kitafanya mkutano mkuu na kuamua namna ya ushirikiano na kwamba vitatoa matakamko kuhusu nafasi hiyo.
Pia amesema wamemsikia Katibu Mwenezi na Itikadi wa Chama Cha Mapinduzi, Humprey Polepole akizungumzia masuala ya rushwa katika chama chake,hivyo wanamuomba lisiishie katika uteuzi tu, bali waendelee hadi kwenye ngazi ya uchaguzi,” alisema Rain a kuongeza:
“Tunataka suala la kupinga rushwa liende hadi kwenye sanduku la kupiga kura, suala la kupita bila kupingwa nalo tutalihesabu kama sehemu ya rushwa kwa sababu haiwezekani mgombea apite bila ya kupingwa,” alisema Rai.
Aidha, ameiomba Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kuhakikisha inakuwa macho katika kuwakamata na kudhibiti vitendo vya baadhi ya wagombea ambao wamejiandaa kutoa rushwa kwa wananchi.
"Rushwa ni mojawapo ya jambo linaloharibu uchaguzi mkuu na kwamba wagombea wasiokuwa na sifa ndiyo wanaochaguliwa kwa kutoa rushwa,"amefafanua.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa umoja huo, Hassan Almas, ameeleza kwamba kila jimbo vyama vyao vitashirikiana kwa kupiga kampeni kwa pamoja na kwamba kila mgombea atakapokuwa anafanya kampeni atakuwa na bendera za vyama vyote.
"Kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu, umoja huo umeamua kusimamisha mgombea kwenye kila jimbo na kwamba watahakikisha mgombea atakayeteuliwa kukiwakilisha chama amechaguliwa na wajumbe wa vyama vyao,"amefafanua.
Wakati huo huo Katibu wa umoja huo, Abdul Mluya, akielezea kuhusu vyama vya siasa kusaini maadili ya uchaguzi ni kwamba walisaini pasipo kulazimishwa, "Sisi tulisaini baada ya kuona maadili yapo vizuri, sasa hao wanaolalamika kwamba walilazimishwa tunawashangaa”.
Amesema walipokuwa wakisaini maadili hayo hakuna chama kilicholazimishwa na baadhi ya vyama wanataka kufanya mchakato wa uchaguzi kuwa ni suala la kwao peke yao jambo ambalo siyo kweli kwani ni suala linalowashirikisha wananchi.
Katibu Mkuu wa Chama cha DP,Abdul Mluya ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Muunganiko wa vyama hivyo 12,akitoa ufafanuzi zaidi kuhusu ni kwa namna gani vyama hivyo vitashiriki katika uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu,ikiwemo pia kuwasimamisha Wabunge na Madiwani kwa kila jimbo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP,Richard Lymo akizungumza wakati wa Mkutano huo,ambapo kupitia chama chao wameamua kutokuwa na Mgombea kwa nafasi ya Rais badala yake wametangaza kumuunga mkono Rais Dkt John Pombe Magufuli katika uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu.
Mkutano ukiendelea na Waandishi wa Habari
Baadhi ya viongozi 12 wa vyama vya siasa visivyo na wawakilishi Bungeni,ambapo kwa pamoja walitamka kushiriki uchaguzi mkuu wa Oktoba 25,2020.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakiendelea wakifuatilia mkutano huo uliofanyika jijini Dar na kuhudhuriwa na viongozi 12 wa vyama vya siasa visivyo na wawakilishi Bungeni,ambapo kwa pamoja walitamka kushiriki uchaguzi mkuu wa Oktoba 25,mwaka huu

No comments: