AZAM FC, TFF KUADHIMISHA SIKU YA UTOAJI DAMU DUNIANI KWA KUCHANGIA DAMU
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
KUELEKEA siku ya utoaji damu duniani Juni 14 kila mwaka, Klabu ya Azam imeungana Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuadhimisha siku hiyo muhimu.
Zoezi hilo la uchangiaji damu linatarajiwa kufanyika nje ya Uwanja wa Azam Complex kuanzia majira ya saa 6 mchana.
Juni 14, Azam itakuwa ikicheza mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) dhidi ya Mbao saa 1.00 usiku na kuhusisha watu wa aina mbalimbali.
Zoezi hilo la uchangiaji damu na kudumisha shirikiano huo kutatanguliwa na mchezo wa kirafiki, utakaowahusisha wafanyakazi wa timu hizo, ukianza majira ya saa 10.00 jioni.
Taarifa iliyotolewa na TFF, imesema kama Shirikiaho iimeona kuna haja ya kushirikiana na Azam FC katika kuadhimisha siku ya utoaji damu Kimataifa siku ya tarehe 14 Juni mwaka huu.
Azam, imeweka Utaratibu kwa watu wote wataojitokeza kuchangia damu katika siku huyo watajipatia tiketi ya bure kushuhudia mechi kati ya Azam FC na Mbao.
Kwa pamoja wametoa wito kwa mashabiki wa mpira na wakazi wa maeneo ya karibu na uwanja wa Azam , kujitokeza kwa wingi kusapoti juhudi za Serikali pamoja na Kitengo cha Damu Salama, katika kutunisha benki ya damu ya Taifa, ili kuokoa maisha ya Watanzania wenzetu wenye uhitaji wa damu hospitalini.
Toa damu, uokoe maisha ya Mtanzania mwenzako!
No comments: