WAZIRI MKUU AFURAHISHWA NA KASI YA UJENZI MRADI MKUBWA WA UMEME WA JULIUS NYERERE WA MW 2115
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Kassim Majaliwa ameridhishwa na hatua mbalimbali za ujenzi wa Mradi mkubwa wa Kufua Umeme kwa maji wa Julius Nyerere (JNHPP) unaotekelezwa kwenye mto Rufiji.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo Mei 14, 2020, baada ya kufanya ziara kwenye eneo la mradi unaotarajiwa kuzalisha jumla ya Megawati 2115“ utakapokamilika 2022.
Waziri Mkuu ambaye alifuatana na Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo mhandisi Zena Said watendaji wa TANESCO wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji TANESCO, Dk.Tito Mwinuka, alisema ziara yake ililenga kupata picha halisi ya hali ya mradi na hatua iliyofikiwa.
“Nimefarijika sana kuona hatua iliyofikiwa toka mradi umeanza mwezi Juni mwaka Jana mpaka leo ni ya kuridhisha.” Alisema Waziri Mkuu.
Alisema ziara yake imempa fursa ya kujionea jinsi kazi zinavyoendelea na nimatumaini yake utakamilika kwa wakati “Nimepata fursa ya kuona eneo lote la mradi na kazi mbalimbali zikiendelea, wakandarasi wanafanya vizuri na sisi Kama Serikali kupitia Wizara na TANESCO tumekuwa karibu nao kuhakikisha wanafanya vizuri na hayo ndio matarajio ya watanzania.” alisema Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu amewahakikishia watanzania kuwa mradi huo utakamilika katika muda uliopangwa na kuwapongeza wakandarasi kampuni ya Elsewedy na Arab contractor kutoka Misri kwa kazi nzuri.
Alisema licha ya changamoto ya mvua za masika bado kazi ya ujenzi iliendelea. Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa ujenzi wa mradi huo Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani alisema, ujenzi ulianza 15/6/2020 na utakamilika 14/6/2022.
“Mradi unashughuli kubwa saba kati ya hizo muhimu sana ni nne, ujenzi wa njia ya kuchepusha maji, kujenga bwawa lenyewe, kujenga kingo nne zitakazowezesha maji kuhifadhiwa na ya mwisho ni kujenga power house.”. alifafanua Dkt. Kalemani.
Dkt.Kalemani alisema Hadi sasa mkandarasi ameshalipwa shilingi trilioni 1.29 ya jumla ya shilingi trilioni 6.5 ya mkataba mzima. “Malipo hayo ni sawa na asilimia 100 ambayo inahusu malipo ya awali asilimia 15 na malipo ya kazi alizofanya Hadi sasa.” Alifafanua Dkt. Kalemani.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (kulia) akiwa na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, akizungumza wakati alipotembeela eneo la ujenzi wa mradi wa umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) wa MW 2115 huko Rufiji Mkoani Pwani Mei 14, 2020.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitazama maendeleo ya ujenzi wa mradi wa kufua umeme wa maji wa Julius Nyerere kwenye mto Rufiji mkoani Pwani Mei 14, 2020.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (katikati, mstari wa mbele) akiongozana na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kushoto) na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Zena Said (kulia) wakati akitembeela ujenzi wa mradi wa umeme wa maji wa Julius Nyerere (JNHPP) kwenye mto Rufiji mkoani Pwani, Mei 14, 2020.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO (Anayeshughulikia Miundombinu na Uwekezaji) Mhandisi Khalid James), akiteta mwakilishi wa kampuni iliyopewa kandarasi ya ujenzi wa mradi wa JNHPP ya El Sewedy Electric kutoka Misri.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Zena Said, akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ziara hiyo.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (kushoto), akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO Dkt. Tito Mwinuka (kulia) mara baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea ujenzi wa mradi wa kufua umeme wa majai wa Julius Nyerere (JNHPP) kwenye bonde la mto Rufiji mkoani Pwani Alhamisi 14/5/2020.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia) akizungumza na wakandarasi wanaotekeleza ujenzi wa mradi wa umeme wa Julius Nyerere, Arab Contractors na Elsewedy kutoka nchini Misri, wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo utakaozalisha MW 2115 za umeme. Waziri Mkuu alitembeela mradi huo Alhamisi 14/5/2020.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (wakwanza kushoto), akiteta jambo na Mkurugenzi qa TANESCO Dkt. Tito Mwinuka (aliyevaa nguo nyeusi), Katibu Mkuu Wizara ya Nishatio Mhandisi Aziza Said (wapili kushoto) na wakandarasi wa kampuni za Arab Contractors na Elsewedy zote kutoka Misri, wakati wa ziara ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kutembelea mradi wa umeme wa maji wa Julius Nyerere (JNHPP) huko Rufiji Mkoani Pwani 14/5/2020.
Taswira ya baadhi ya maeneo ya ujenzi wa mradi wa JNHPP leo Mei 14, 2020
Taswira ya baadhi ya maeneo ya ujenzi wa mradi wa JNHPP leo Mei 14, 2020.
No comments: