TAASISI YA BMF YAENDESHA MAFUNZO KWA WAHUDUMU WA AFYA NGAZI YA JAMII UMMY ASHAURI TUJIFUNZE KUISHI NA CORONA
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii
WAZIRI wa Afya, maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto, Ummy Mwalimu amewaasa Watanzania kujifunza kuishi na Corona kwani itakuwepo kwa miezi kadhaa hivyo maisha ni lazima yaendelee na uzalishaji mali uendelee huku wananchi wakiendelea kuchukua tahadhari kwa kufuata miongozo iliyotolewa na waudumu wa afya.
Ameyasema hayo leo Mei 14, 2020 jijini Dar es Salaam alipotembelea mafunzo ya waudumu wa afya ngazi ya jamii yanayotolewa na Wizara ya afya kwa ufadhili wa Taasisi ya Benjamin Mkapa (BMF) kwa kushirikina na Unicef na Taasisi ya Irish Aid ya Ireland.
Amesema, Mafunzo kwa ajili ya waudumu wa afya wa ngazi wa jamii ni sehemu y mikakati ya serikali ya kuboresha na kutatua changamoto za afya nchini ambapo tulifanya maamuzi ya kutumia waudumu wa afya ngazi ya jamii kwa sababu wako katika jamii ili waweze pia kushiriki katika mfumo mzima wa utoaji wa huduma za afya.
Amesema kwa sasa muundo mzima wa utoaji huduma za afya hautakuwa ukianzia kwenye zahanati, utakuwa unaanzia kwenye ngazi ya jamii ambapo kutakuwa na hao wahudumu wa afya ngazi ya jamii.
" Tulizindua mpango huu Aprili 17 mwaka huu, leo nafurahi kuona tunaanza utekelezaji wa mpango wa serikali wa kuwatumia wahudumu wa afya ngazi ya jamii katika mfumo mzima wa utoaji wa huduma za afya.
Waziri Ummy pia amepongeza katika mapambano hayo dhidi ya Corona COVID19 serikali imepata waudumu wa afya ngazi ya jamii ambao watakuwa wanashiriki moja kwa moja katika mapambano dhidi ya corona hususani jukumu lao likiwa ni kufuatilia tetesi za watu wanaoumwa ugonjwa wa Corona na pia kwenda kuwapa ushauri pamoja na kuwasaidia kupata raarifa sahihi ya jinsi ya kujikinga ama kujilinda na ugonjwa wa Corona.
Katika mafunzo hayo jumla ya waudumu wa afya wapatao 620 wamepewa mafunzo ambapo sasa kila mtaa wa jiji la Dar es salaam angalau kutakuwa na muudumu mmoja wa afya ngazi ya jamii ambao wanajulikana kama afya Komando.
Aidha ameta eneo la Ubungo kutakuwa na waudumu wa afya 90 Ilala 184, Kigamboni, 59, Kinondoni 129 na Temeke 158.
Hawa walikuwa wakijitolea katika mitaa yao hivyo wana moyo ari na hamasa ya kutumikia jamii. waudumu wa afya katika ngazi ya jamii watatoka katika jamii husika, kwa kutumiwa na waudumu wa afya kwenye ngazi ya jamii tutapata watu wanaokubalika na jamii, kueleweka na jamii na kushaurika katika jamii husika,hatutaishia Corona tu, tutawatumia pia katika miradi mbali mbali ya afya, watakuwa wakifanya kazi chini ya Afisa afya wa kata.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Benjamin Mkapa (BMF) Dk. Ellen Mkondya amesema, mafunzo waudumu hao wa afya wamepatiwa mafunzo na wizara ya afya kwa kupata muongozo ambao umepitishwa na wizara na pia wanashiriana na maafisa afya wa ngazi ya kata ambao ndio watakuwa wanawasimamia katika kazi zao.
Amesema Taasisi ya enjamin Mkapa baada nakuona janga la Corona limejitokeza nchini wamejitahidi kuwa mstari wa mbele katika kupambana nalo amapo wamekuwa wakishirikiana na idara ya ufuatiliaji na elimu ya afya kwa umma.
"Kwa kushirikina na wizara ya afya tumeweza kupata fedha za ufadhili kutoka Shirika la UNICEF pamoja na Taasisi ya Irish Aid kutoka ubalozi wa Ireland ambao wametusaidia katika kuajiri na kuwatafuta watu wanaojitolea kuhudumia afya katika ngazi ya jamii wapata 620"amesema Dk. Ellen.
Ameongeza kuwa watawasaidia waudumu hao waliopatiwa mafunzo kwa kuwapatia motisha kwa muda wa miiezi mitatu ya mwamwanzo na wengine wataenda hadi miezi sita huki wakiendelea kuangalia hali halisi ya maambukizi ya Corona na katika kipindi chote hicho washiriki watapatiwa vifaa mbalimbali vitakavyowawezesha katika kufanya kazi zao na kujikinga wakati waufuatiliaji wa wagonjwa majumbani na kutoa takwimu zitakazokuwa zinaenda katika ngazi ya mkoa hadi ngazi ya wizara.
Aidha waziri Ummy ameishukuru Taasisi ya Benjamini Mkapa, Irish Aid na UNICEF na kuwaomba wadau wengine kuendelea kushirikina na serikali katika kupambana na gonjwa hili hatari ya homa ya mapafu ya Corona kwani serikali peke yake hatuwezi janga hili linahitaji ushiriki wa kila mmoja.
Naye mshiriki wa mafunzo hayo, Daniel Mayir ambaye ni muudumu wa ngazi ya jamii, ameshukuru kupatiwa mafunzo hayo na kusema yatamsaidia kuweza kutoa elimu mtaani na kwa jamii nzima ili kuweza kupambana na janga la Corona ambalo bado linaitesa dunia nzima.
"Tutawapa elimu ya kuweza kujikinga kwa kuzingatia vigezo vitatu muhimu sana ambavyo ni kunawa maji kwa sabuni kwa kutumia maji yanayotiririka, kuepuka mkusanyiko na kuvaa barakoa" amesema Mayir.
Nae Ramlat Omary ameshukuru sana kupatiwa Taasisi ya Benjamini Mkapa kuwapatia mafunzo hayo na kuahidi kutoa elimu kwa wananchi na kuwaondolea hofu kwani ugonjwa huu ukichukua tahadhari unaweza kuepuka kwa kufuata miongozo ya inayotolewa na wataalamu wa afya.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Benjamini Mkapa (BMF), Dk. Ellen Senkoro akizungumza wakati wa kukabidhi na kutoa mafunzo wa wahudumu wa afya ngazi ya jamii yanayofanyika shule sekondari Kibasila 'B' Temeke jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza na wahudumu ngazi ya jamii ikiwa ni mkakati wa pamoja na kuimarisha ufuatiliaji wa tetesi za wagonjwa na watu waliokua karibu na wagonjwa wa COVID-19.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akikabidhi vitendea kazi mmoja wa wahudumu wa afya ngazi ya jamii, Ramlat Omary wakati wa mafunzo yaliyohusu utambuzi na ufuatiliaji wa homa kali ya mapafu katika ngazi ya jamii kwa wilaya ya Temeke.
Mkurugenzi Msaidizi, Kitengo cha Ufatiliaji wa magonjwa, Janeth Gamba
akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa mafunzo ya wahudumu wa afya ngazi ya Jamii.
Mafunzo yakiendelea katika madarasa ya Shule ya Sekondari Kibasira 'B' Temeke jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasiri katika shule ya Sekondari ya Kibasila jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwasiri katika shule ya Sekondari ya Kibasila 'B'
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza na wahudumu wa Afya kazi ya jamii leo wakati wakipata mafunzo ya kuhudumia jamii.
No comments: