WAZIRI BASHUNGWA AWATOA HOFU WATANZANIA KUHUSU UHABA WA SUKARI NCHINI,AWATAKA WAFANYA BIASHARA KUZINGATIA BEI ELEKEZI

Na. Eliud Rwechungura – Wizara ya Viwanda na Biashara.

Waziri wa viwanda na Biashara Mhe.Innocent Bashungwa (Mb) amewahakikishia watanzania kuwa hakutakuwa na uhaba wa sukari tena na kuwataka wananchi wasiwe na hofu juu ya sukari na kuwahasa wauzaji kuzingazia bei elekezi.

Mhe.Bashungwa ameyasema hayo jana Mei 14, 2020 alipofika katika bandari ya Mwanza kusini na kushuhudia Shehena ya Sukari tani 20,000 ikishushwa na meli kutoka Nchini Uganda iliyoagizwa na kiwanda cha kagera sugar kwa ni niaba ya Serikari

Mhe.Bashungwa baada ya kujionea sukari ya ikishushwa amempongeza Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella na uongozi mzima wa mkoa mwanza kwa kusimamia zoezi vizuri na kwa uharaka sana;

‘‘Nakupongeza Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella na uongozi mzima wa mkoa mwanza kwa kusimamia zoezi vizuri na kwa uharaka sana kwa sababu kila mwaka viwanda vyetu vya ndani vinaposimisha uzalishaji kwa ajili ya ukarabati wa mitambo huwa ilaleta changamoto lakini amemshukuru Rais Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli kwa kutambua hilo na kuona ni kipindi ambacho ndugu zetu Waislamu wapo kwenye mfungo wa Mwezi mtukufu wa ramadhani na kipindi hiki ambacho nchi na dunia inapambana na janga la Corona kuhakikisha upatikanaji wa Sukari kila mahali nchini na kwa kuzingatia bei elekezi’’

Aidha Mhe. Bashungwa amewatoa hofu watanzania kwa kuwahakikishia kuwa tatizo la sukari lilikuwepo limeisha kuanzia leo kwa sababu sukari ya kutosha imeshaagizwa na tiali imefika nchi na inaendelea kusambazwa kwenye mikoa mbalimbali

‘‘Watanzania wote nawaomba muendelee na mwezi mtukufu wa ramadhani vizuri Serikali tunahangaika ili kuhakikisha sukari inapatikana mikoa yote na kupanda kwa bei hakutakuwepo na niendelea kutoa wito kwa wakuu wa mikoa na Wilaya kuendelea kusimamia ukomo wa bei ambao ulitolewa na Serikali na kuhakikisha kila mtanzania anapata sukari bila bugudha yoyote ile,"alisema Mhe.Bashungwa.

Ameendelea kusisitiza kuwa ‘‘Sasa hivi tumejionea Tani 20,000 zikishushwa hapa Mwanza pia na Dar es salaam tunaendelea kushusha sukari maana tuliitoa vibari vya Tani 40,000 na kampuni zilizopewa hivyo vibari mpaka sasa kampuni hizo zinaendelea kushusha sukari’’

Naye wakala wa usambazaji Sukari kanda ya ziwa Pravin Shah amesema hakutakuwa foleni tena wala uhaba wa sukari kwa sasa kwani sukari iliyoaagizwa imeshafika na ipo ya kutosha

"Kwa sasa hakuna uhaba wa sukari hata ukitaka mifuko elfu moja utapata na kwa bei ni elekezi iliyowekwa na Serikali maana sukari imeshafika nchi na inaendelea kushushwa na kusambazwa kote" alisema Pravin Shah.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella amesema kama Mkoa umejipanga vizuri ili kuhakikisha sukari inayoendelea kushushwa inawafikia wananchi kwa bei elekezi bila.

Waziri wa viwanda na Biashara Mhe.Innocent Bashungwa akiwa Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe. John Mongella wakikagua magari yaliyobeba Sukari ambayo inaendelea kusambazwa katika mikoa mbalimbaili. Mwanza – 14.05.2020.
Waziri wa viwanda na Biashara Mhe.Innocent Bashungwa (aliyebeba gunia la sukari} akiwa na Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe. John Mongella wakishiriki katika zoezi ya kushusha Shehena ya Sukari ya Tani 20,000 iliyofika bandari ya Mwaza kusini kwa meli kutoka Nchini Uganda. Mwanza – 14.05.2020 {Picha na Eliud Rwechungura – Wizara ya Viwanda na Biashara}.
Wafanyakazi wa bandali ya Mwanza kusini wakiendelea kushusha Tani 20,000 za sukari ambayo inapakiwa kwenye magari kwa ajili ya kusambazwa mikoa mbalimbali, jijini Mwanza jana.

No comments: