KAMPUNI YA GVEN WEAR YATOA MSAADA WA BARAKOA KWA KAYA ZINAZOISHI MAZINGIRA MAGUMU MANISPAA YA SHINYANGA
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kampuni ya Ushonaji Nguo na Mitindo Gven Wear ya Mkoani Shinyanga imetoa msaada wa Barakoa 100 kwa kaya zinazoishi katika Mazingira Magumu katika Manispaa ya Shinyanga ili kujikinga na Maambukizi dhidi ya Virusi vya Corona ‘COVID 19’.
Zoezi la kutembelea kaya hizo na kukabidhi barakoa kwa walengwa limefanyika leo Alhamis Mei 14,2020 likiendeshwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Gven Wear Bi. Grace Mng’ong’o aliyekuwa ameambatana na Wenyeviti wa Serikali za mitaa wakiongozwa na Mwenyekiti wa Wenyeviti wa serikali za Mitaa Manispaa ya Shinyanga Bw. Nassor Warioba.
Kampuni ya Gven Wear imegawa barakoa 100 katika mitaa ya Sanjo na Chamaguha iliyopo katika kata ya Chamaguha, mtaa wa Viwandani uliopo kata ya Mjini na mtaa wa Ibinzamata uliopo katika kata ya Ibinzamata.
Akizungumza wakati wa kukabidhi barakoa hizo, Mng’ong’o amesema Kampuni hiyo imeona ni vyema kuzifikia kaya ambazo hazina uwezo ili nazo zisiwe nyuma katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona.
“Kampuni ya Gven Wear ambayo inajihusisha na ushonaji wa nguo imepata msukumo wa kutengeneza Barakoa za vitambaa na kuzigawa kwa kaya zenye watu wenye uhitaji,hususani wazee ambao hawana hata uwezo wa kununua barakoa ili wazitumie kujikinga dhidi ya maambukizi ya Corona”,amesema Mng’ong’o.
“Wakati tukiendelea na zoezi la kugawa hizi barakoa tukishikiriana na wenyeviti wa serikali za mitaa tumetoa elimu namna ya kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona kama vile imekuwa ikielekezwa na Watalaamu wa afya ikiwemo kuvaa barakoa,kunawa maji tiririka na sabuni, kutokumbatiana na kuepuka mikusanyiko”,ameongeza Mkurugenzi huyo wa Kampuni ya Gven Wear.
Hata hivyo Mng’ong’o amesema Kampuni yake itaendelea kusaidia jamii zenye uhitaji kadri itakavyowezekana ili kuhakikisha kuwa hakuna mtu anayeachwa nyuma katika mapambano dhidi ya Virusi vya Corona.
Wakizungumza wakati wa kupokea barakoa hizo,wananchi hao wameishukuru Kampuni ya Gven Wear kwa kuwajali huku wakibainisha kuwa watazitumia barakoa hizo kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona.
“Tunamshukuru sana kwa msaada huu, Mungu amuongezee zaidi pale alipotoa.Tunaomba wadau wengine waje kutuletea sabuni na ndoo za kunawia mikono kwani hatuna uwezo wa kununua”,alisema Bi. Kwangu Lung’wecha na Mzee Furaha Lukeyemba Mdandi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wenyeviti wa serikali za Mitaa Manispaa ya Shinyanga Bw. Nassor Warioba ambaye ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Miti Mirefu kata ya Mjini ameishukuru Kampuni ya Gven Wear kwa kuzifikia kaya zinazoishi katika mazingira magumu huku akiwataka wadau wengine kujitokeza kusaidia watu wenye uhitaji.
“Ninamshukuru sana ndugu yangu Grace Mng’ong’o kwa kuguswa na hali ya maisha ya baadhi ya wananchi ambapo yeye kaona ni vyema akazitembelea familia hizi za watu wa hali ya chini ambazo hazina hata uwezo wa kununua barakoa,yeye kaamua kutembea na kutoa barakoa kwa mkono wake. Ninamshukuru sana”,amesema Warioba.
“Namshukuru pia kwa kutambua nafasi ya viongozi wa serikali za mitaa ambao kimsingi ndiyo wanawajua wananchi wote katika mitaa. Alinishirikisha kuhusu jambo hili zuri nami nikawashirikisha wenyeviti wenzangu wa mitaa ambao tumekuwa nao mtaa kwa mtaa kufanikisha zoezi hili la kugawa barakoa kwenye familia zenye uhitaji”,ameongeza Warioba.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkurugenzi wa Kampuni ya Gven Wear Bi. Grace Mng’ong’o akimpa barakoa mkazi wa mtaa wa Sanjo kata ya Chamaguha katika Manispaa ya Shinyanga leo Alhamis Mei 14,2020. Aliyesimama kulia ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Sanjo, Bw. Elias Ramadhan. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kushoto ni Mwenyekiti wa Wenyeviti wa serikali za Mitaa Manispaa ya Shinyanga Bw. Nassor Warioba akitoa elimu namna ya kujinga na Maambukizi ya Corona kwa mkazi wa mtaa wa Sanjo (aliyekaa kushoto) wakati Mkurugenzi wa Kampuni ya Gven Wear Bi. Grace Mng’ong’o akitoa msaada wa barakoa kwenye familia/kata zinazoishi katika mazingira magumu.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Gven Wear Bi. Grace Mng’ong’o akimpa barakoa mkazi wa mtaa wa Sanjo kata ya Chamaguha.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Gven Wear Bi. Grace Mng’ong’o akiendelea kugawa barakoa.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Gven Wear Bi. Grace Mng’ong’o akiendelea kugawa barakoa.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Gven Wear Bi. Grace Mng’ong’o akimsititiza mkazi wa mtaa wa Sanjo kata ya Chamaguha kuepuka kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni mara kwa mara na kuepuka mikusanyiko ya watu.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Gven Wear Bi. Grace Mng’ong’o akimuangalia mkazi wa mtaa wa Sanjo anavyovaa barakoa.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Gven Wear Bi. Grace Mng’ong’o akimwelekeza mkazi wa mtaa wa Sanjo kata ya Chamaguha namna ya kuvaa barakoa.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Gven Wear Bi. Grace Mng’ong’o akimpa barakoa Mzee Furaha Lukeyemba Mdandi mwenye umri wa miaka 100 mkazi wa mtaa wa Chamaguha kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga ili kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Gven Wear Bi. Grace Mng’ong’o akigawa barakoa kwa wakazi wa mtaa wa Chamaguha kata ya Chamaguha.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Gven Wear Bi. Grace Mng’ong’o akimpa barakoa mkazi wa mtaa wa Chamaguha kata ya Chamaguha.
Kushoto ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Chamaguha kata ya Chamaguha, Hussein Matamba akitoa elimu ya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona kwa mwananchi wa mtaa wake.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Gven Wear Bi. Grace Mng’ong’o akigawa barakoa kwa mkazi wa mtaa wa Viwandani kata ya Mjini. Aliyesimama kushoto ni Mwenyekiti wa mtaa wa Viwandani Bw. Ashiraf Majaliwa akishuhudia zoezi la ugawaji barakoa.
Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Gven Wear Bi. Grace Mng’ong’o akimkabidhi barakoa Mwenyekiti wa mtaa wa Viwandani Bw. Ashiraf Majaliwa ili azigawe kwenye kaya/familia zenye uhitaji katika mtaa huo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Gven Wear Bi. Grace Mng’ong’o akimpa barakoa mkazi wa mtaa wa Ibinzamata kata ya Ibinzamata.
Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Gven Wear Bi. Grace Mng’ong’o akimkabidhi barakoa Mwenyekiti wa Mtaa wa Ibinzamata Mohammed Mustapher Mgendi ili azigawe kwenye kaya/familia zenye uhitaji katika mtaa huo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Gven Wear Bi. Grace Mng’ong’o akizungumza wakati wa kukabidhi barakoa 100 katika mitaa ya Sanjo na Chamaguha iliyopo katika kata ya Chamaguha, mtaa wa Viwandani uliopo kata ya Mjini na mtaa wa Ibinzamata uliopo katika kata ya Ibinzamata.
Mwenyekiti wa Wenyeviti wa serikali za Mitaa Manispaa ya Shinyanga Bw. Nassor Warioba ambaye ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Miti Mirefu kata ya Mjini akiishukuru Kampuni ya Gven Wear kwa kuzifikia kaya zinazoishi katika mazingira magumu huku akiwataka wadau wengine kujitokeza kusaidia watu wenye uhitaji.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog.
No comments: