WANANCHI WATAKIWA KUACHA KUPUUZIA UGONJWA WA CORONA KWANI UPO NA UNAUWA
*******************************
Na Woinde Shizza , KILIMANJARO
Diwani wa kata ya Bomambuzi iliopo ndani ya manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro Juma Rahib amewataka wananchi kuacha kupuuzia ugonjwa huu wa Corona kwani upo na unauwa hivyo ,amewataka watanzania wote kuendelea kuchukuwa tahathari kwa kufuata maelekezo yote yanayotolewa na wataalam wa Afya.
Aidha pia aliwaonya baadhi ya watu ambao wanajitokeza katika sehemu mbalimbali ikiwemo Mkoani Kilimanjaro na kudai kuwa wamevumbua dawa ya kutibu ugonjwa huu wa Corona 19 wakati dawa zao hazijachunguzwa na kuhizinishwa na Serikali kwa ajili ya matumizi ya binadamu.
Aliyasema hayo juzi wakati akikabidhi vifaa kwa ajili ya kujikinga na ugonjwa huo katika taasisi baadhi za Serikali ikiwemo kituo Cha Kati polisi Moshi mjini,mahakama,ofisi za manispaa ya Moshi,soko la Pasua ,Standi kuu ya mabasi pamoja na kituo Cha afya Cha Pasua ambapo aliweza kukabidhi mapipa ya kunawia mikono 15 yenye thamani ya shilingi milioni moja laki mbili,barakoa 1000 pamoja na vitakasa mikono (sanitaiza)100.
Alibainisha kuwa Kuna baadhi ya wananchi wanapuuzia ugonjwa huu na kuacha kuvaa barakoa ,wengine wanavaa lakini hawafati kanuni za uvaaji kwani wengine wanavaa wanaacha pua wazi ,wengine wanavua barakoa wakati wakiongea Jambo ambalo ni hatari Sana katika maisha Yao pamoja na Afya zao kwa ujumla.
” niwaombe wananchi wa manispaa ya Moshi tuendelee kunawa mikono kwa kutumia maji tiririka na sabuni,tuvae barakoa lakini pia tuendelee kufuata taratibu na maelekezo yote yanayotolewa na ndugu zetu wataalam wa afya pamoja na Serikali yetu kwa ujumla”alisema Juma
Pia alitoa maelekezo kwa jeshi la polisi mkoa wa Kilimanjaro kuendelea kuwakamata wale wote ambao wanatengeneza dawa za corona ambazo azijafanyiwa uchunguzi na kuhizinishwa na serikali ,kwani hata Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli alipo agiza dawa kutoka nchini Madagasca zilipofika aliagiza dawa zile kutokutumika hadi pale zitakapo fanyiwa uchunguzi wa kubaini Kama hazitaleta madhara kwa binadamu.
“Kunawatu wameibuka kipindi hichi wanalala nyumbani kwao wakiamka wanasema wamezindua dawa ya Corona ,dawa ambazo hazijachunguzwa atujui Zina madhara gani ,nasema hivi Kama mtu kazindua dawa na anataka itumike ni lazima afuate Sheria kwa kuchukuwa dawa yake na kupeleka sehemu husika za uchunguzi ikiwemo TFDA,TBS ,NIMRI pamoja na kwa wataalam wa tiba asili kabla ya kuanza kuitangaza na kuitoa kwa wananchi ,kwani atuwezi leo tukafa na Corona na kesho tukaanza kuuliwa na dawa kutoka mitaani “Alibainisha Juma
Aidha aliwataka baadhi ya watu wanaopotosha Uma na kutoa taarifa za uongo juu ya idada ya wagonjwa ,idadi ya vifo ,na idadi ya maambukizi ya wagonjwa wa ugonjwa huu wa Corona kuacha Mara moja kwani wanavyofanya hivyo wanaleta taaruki katika jamii ,huku akisisitiza kuwa sio kila kifo kinachotokea kipindi hichi kinasababishwa na ugonjwa huo Bali Kuna magonjwa mengine pia aliwakumbisha wananchi kuwa taarifa pekee ambazo wanatakiwa kuamini ni zile zinazotolewa na waziri mwenye zamana ,waziri mkuu Kasim Majaliwa pamoja na Rais John Magufuli tu na sio Mwingine.
Akipokea msaada huo mganga mkuu wa manispaa ya Moshi Mgeta Sebastian alisema msaada huu ni muhimu Sana kwao hasa ukizingatia katika kipindi hiki Cha mapambano dhidi ya ugonjwa hatari wa Corona ambao umetikisa dunia na unaendelea kuitikisa Hadi Sasa.
Alisema watatumia msaada huu katika maeneo husika kwakuwa hata vifaa vya kunawia mikono vilivyotolewa vinaujazo mkubwa hivyo watavielekeza katika maeneo ya mikusanyiko ya watu Kama vile Standi ,mahospitali pamoja na masokoni ,ambapo aliwataka Wadau mbalimbali kuendelea kutoa misaada ili kuweza kuendelea kuungana kutokomeza ugonjwa huu.
5057 Diwani wa kata ya Bomambuzi Juma Rahib kushoto akikabithi mkuu wa kituo Cha polisi Kati Moshi mjini Elizabeth Mlela pipa kwa ajili ya kunawia mikono wananchi pamoja na Askari wote wanaoingia kituoni hapo ,ambapo mkuu huyo wa kituo was kituo alisema msaada huo utasaidia kujikinga na ugonjwa wa Corona ambao umekuwa ni tatizo kubwa dunia mzima , Aliwaomba Wadau mbalimbali kuiga mfano wa diwani huyu (picha na Woinde Shizza, Kilimanjaro)
No comments: