BARAZA LA MADIWANI NYASA LAMPONGEZA NAIBU WAZIRI MANYANYA

Mbunge wa wa Jimbo la Nyasa Mhandisi Stela Manyanya Amabaye pia ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara akiwa katika Baraza la Madiwani lililofanyika katika Ukumbi wa Kepten John Komba Mbamba-bay Wilayani Nyasa.Pamoja na mambo mengine Baraza hilo limempongeza kwa kutekeleza miradi mingi ya Maendeo Wilayani hapa

*********************************

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa, limempongeza Mbunge wa jimbo la Nyasa ambaye pia ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stela Manyanya kwa kutatua changamoto mbalimbali za jimbo la nyasa ikiwemo kukabidhi gari jipya la kubeba wagonjwa la kituo cha afya Mbamba-bay.

Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa, Mh. Alto Komba wakati Akizungumza kwa niaba ya madiwani wote wa Wilaya ya Nyasa katika baraza la Madiwani la Wilaya ya Nyasa lililofanyika katika Ukumbi wa Kepten John Komba ,mbamba-bay Wilayani hapa.

Bw Komba alifafanua kuwa, Baraza la Madiwani Wilayani hapa linampongeza sana Mh Mbunge wa Nyasa kwa kazi nyingi na nzuri, za kutatua changamoto nyingi zilizokuwa zinaikabili Wilaya ya Nyasa, Miradi ya Maendeleo imetekelezwa vizuri na kila Kata imepewa Miradi
mikubwa .

“Mh Mbunge Baraza la Madiwani linakupongeza sana kwa juhudi zako za kuifanya Nyasa iwe juu.Miradi ya maendeleo imetekelezwa kwa kiwango kikubwa na hii leo umetukabidhi gari ya kubebea wagonjwa la kituo cha Afya Mbamba-bay mh, Mbunge wetu tunakushukuru sana
lakini kuna miradi mikubwa iliyoletwa na Serikali kwa kuwa wewe ni mwakilishi na tulikutuma ukaombe, tunakupongeza kwa dhati kwa kutuletea miradi ya Baraba,umeme,maji, ujenzi wa Vituo Vitatu vya afya yaani Mkili, Kingerikiti, na Kihagara na na miradi mingine mikubwa ya Elimu ” .

Aliongeza kuwa Kituo cha afya Mbamba-bay kilikuwa na gari la zamani ambalo lilikuwa ni bovu na lilikuwa likipata changamoto ya matengenezo mara kwa mara, lakini kwa sasa gari hii mpya itawasaidia wananchi wa Wilaya ya Nyasa kufuata Matibabu kokote iwapo itatokea dharula.

Aidha alimuomba mh.Mbunge kufikishia kwa dhati salamu na Pongezi kwa Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kutatua kero za Wananchi wa Wilaya ya Nyasa kwa kuwa awali hawakuwa na miradi mikubwa ya kimkakati kama ilivyo
sasa.

Akizungumza katika Baraza hilo Mbunge wa Jimbo la Nyasa, mhandisi Stela Manyanya, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Alisema analishukuru Baraza la madiwani, kwa ushirikiano waliompa kwa kuwa yeye peke yake asingeweza kuyafikia mafanikio aliyoyopata.

Aliongeza mafanikio haya yametokana nma ushirikiano uliopo kati ya Wananchi, Madiwani, Mkurugezi Mtendaji wa Halmashauri na Mkuu wa wilaya ya Nyasa. Amewaagiza
wananchi kuitunza miradi ya maendeleo iliyopo katika maeneo yao.

No comments: