JESHI LA POLISI LAPOKEA VIFAA KINGA DHIDI YA CORONA.








Kamishna wa Polisi, Kamisheni ya Uchunguzi wa Kisayansi CP Shaban Hiki akipokea vifaa kinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona kutoka kwa Balozi wa kampeni ya Mikoni safi, Tanzania salama, Msanii Mrisho Mpoto (Mjomba), tukio lililofanyika katika makao makuu Jeshi la Polisi Ofisi ndogo Jijini Dar es Salaam.



Timu ya uhamasishaji kutoka Wizara ya Afya na Wadau kutoka Shirika lisilo Lakiserikali la Project CLEAR wakimsikiliza Kamishna wa Polisi, Kamisheni ya Uchunguzi wa Kisayansi CP Shaban Hiki katika ofisi yake iliyo katika ofisi ndogo za Jeshi hilo makao makuu Jijini Dar es Salaam.



Picha ya pamoja ikiongozwa na Kamishna wa Polisi, Kamisheni ya Uchunguzi wa Kisayansi CP Shaban Hiki na timu yake, pamoja na Timu ya uhamasishaji kutoka Wizara ya Afya na Wadau kutoka Shirika lisilo Lakiserikali la Project CLEAR wakionesha ishara ya kuipiga teke Corona kama sehemu ya hamasa ya mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

Kamishna wa Polisi, Kamisheni ya Uchunguzi wa Kisayansi CP Shaban Hiki akipokea vifaa kinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona kutoka kwa Balozi wa kampeni ya Mikoni safi, Tanzania salama, Msanii Mrisho Mpoto (Mjomba), tukio lililofanyika katika makao makuu Jeshi la Polisi Ofisi ndogo Jijini Dar es Salaam. Picha ya pamoja ikiongozwa na Kamishna wa Polisi, Kamisheni ya Uchunguzi wa Kisayansi CP Shaban Hiki na timu yake, pamoja na Timu ya uhamasishaji kutoka Wizara ya Afya na Wadau kutoka Shirika lisilo Lakiserikali la Project CLEAR baada ya makabidhiano ya vifaa kinga dhidi ya ugonjwa wa Corona.



********************************

Na WAMJW- DSM

Jeshi la Polisi Makao makuu, Ofisi ndogo Dar es Salaam limepokea lita 100 za vipukusi (sanitizers) pamoja na dispenser 5, ikiwa ni sehemu ya vifaa kinga vitavyosaidia kujikinga dhidi ya maambukizi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona.

Akipokea msaada huo kutoka timu ya uhamasishaji kampeni ya “Mikono Safi, Tanzania Salama”, Kamishna wa Polisi, Kamisheni ya Uchunguzi wa Kisayansi CP Shaban Hiki amesema kuwa, msaada huo umekuja wakati sahihi, kutokana na jeshi hilo kuwa na shughuli nyingi zinazowaweka kwenye hatari ya kupata maambukizi.

“Jeshi la polisi lina majukumu mengi ambayo yanawaweka maafisa wake katika hatari za kupata maambukizi ya virusi vya Corona, hivyo kudai kuwa msaada huu kutoka Wizara ya Afya na Wadau wenu wa CLEAR Project umekuja wakati sahihi ” alisema.

Aidha, CP Shaban Hiki ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kuona umuhimu mkubwa wa kulisaidia jeshi hilo, hali inayoongeza kujiamini katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku ya kuwahudumia wananchi.

“Sisi msaada wenu tunauthamini sana, hata kama utakuwa mdogo kiasi gani lakini kwetu utakuwa na msaada mkubwa sana, mfano kwa wenzetu wa mikoani Mbeya na Songwe wanaenda kwenye matukio mengi sana ya mipakani, kwahiyo msaada huu kwetu ni muhimu sana” alisema.

Aliendelea kusema kuwa, hata katika makao makuu uhitaji ni mkubwa sana, akitoa mfano katika kamisheni anayoongoza kumekuwa na utoaji wa hati ya tabia njema za watu wanaoomba kazi katika taasisi mbali mbali na Idara na kuwachukua vidole ili kujua uhusika wa mtu katika uharifu siku za nyuma.

Mbali na hayo, CP Shaban Hiki ametoa wito kwa Wadau wengine kujitokeza kutoa msaada zaidi wa vifaa kinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona kwa jeshi hilo ili kuendelea kulilinda dhidi ya virusi hivyo.

Nae, Mkuu wa Kitengo cha maji na usafi wa mazingira, Wizara ya Afya, Ndg. Anyitike Mwakitalima ameweka wazi kuwa, ugonjwa huu hauna tiba wala chanjo, huku akisisitiza kinga ndio njia pekee inayoweza kuisaidia jamii, likiwemo jeshi kupambana dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona.

“Ugonjwa huu mpaka sasa hivi hauna tiba maalum, wala chanjo, kikubwa ambacho tunatakiwa kufanya ni kuzingatia kinga, kinga ndio kila kitu kwa sasa” alisema.

Aliendelea kusema kuwa, Serikali kupitia Wizara ya Afya na Wadau wake itaendelea kulisaidia jeshi hilo, kwa kuendelea kugawa vifaa kinga dhidi ya maambukizi ya Corona kwa makamanda wa mikoa ili waendelea kujiandaa.

Kwa upande wake Balozi wa kampeni ya Mikoni safi, Tanzania salama, Msanii Mrisho Mpoto (Mjomba) amesisitiza wananchi kupata taarifa kwenye vyanzo sahihi ili kuepusha upotoshaji wa taarifa ambao unaweza zua hofu na taharuki kwa wananchi.

No comments: