UTENDAJI KAZI WA KAMISHNA GENERALI WA JESHI LA MAGEREZA WAMKOSHA RAIS JOHN MAGUFULI

Na Said Mwishehe, Michuzi TV

UTENDAJI kazi unaofanywa na Kamishna Genereli wa Magereza Suleiman Mzee umeonekana kumkosha Rais Dk.John Magufuli ambapo amesema anafanya kazi nzuri sana na wakati mwingine amekuwa akimuona ameshika kileo kwa ajili ya kuchimba mchanga akishirikiana na wafungwa.

Akizungumza leo Mei 21 mwaka huu, akiwa katika Ikulu ya Chamwino Mjini Dodoma, Rais Magufuli amesema kuwa alifanya mabadiliko ya Kamishna Generali wa Magereza na kwamba aliyeko sasa anafanya kazi sana.
"Nilifanya mabadiliko ya Kamishna Jenerali wa Magerezai, yule bwana si yuko hapa, leo hayuko, anafanya kazi, mara leo anapiga koleo, anajaza mchanga kwenye tipa na wafungwa.

"Lakini katika kipindi cha miezi mitatu hajaomba fedha ya kulisha Magereza, wale waliokuwepo wa vyeo vyeo walikuwa wanamsumbua kidogo, akandika barua na huku ikachelewa , baadae nikamwambia Katibu Mkuu Kiongozi shughulikia hilo.

"Anafanya kazi, nasema anafanya kazi, hapo Magereza ameshapanda mpaka mikorosho, waliouwepo hapo awali wala hawakufanya hivyo, lazima iseme ili kusudi tunakoenda tukatimize yale ambayo watanzania wanapenda, mtu anayekupenda atakwambia ukweli , mtu ambaye hakupendi hakuelezi,"amesema Rais Magufuli.

Hivyo ametumia nafasi hiyo kuhimiza waliopata afasi kutekeleza majukumu yao kikamilifu wakiwemo wale ambao amewaapisha leo
Mwisho ambapo wamo mabalozi watatu ambao watakwenda kuwakilisha nchi yetu.

"Kwa hiyo ni matumaini makubwa hata ninyi mabalozi watatu ambao mmeteuliwa mtakwenda kufanya kazi,"amesisitiza Rais Magufuli.
Wakati huo huo ametumia nafasi hiyo kumtaka Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuendelea kufanya kazi na hakuna sababu ya kupunguza kasi yake katika utendaji.

Amesema kuwa Kamishna huyo alikuwa anaikaimu kwa muda mrefu na sasa amempa nafasi hiyo, hivyo hatarajii baada ya kupata nafasi hiyo kurudi nyuma na badala yake aatarajia kumuoa akifanya kazi ya kupambana na kukomesha rushwa nchini.

No comments: