UPELELEZI KATIKA KESI YA KUKUTWA NA DAWA ZA KULEVYA ZAIDI YA KILO 270 INAYOMKABILI RAIA WA NIGERIA, WATANZANIA WAWILI BADO HAUJAKAMILIKA


Na Karama Kenyunko, Michuzi TV

UPELELEZI katika kesi ya kukutwa na dawa za kulevya zaidi ya kilo 270 inayomkabili Raia wa Nigeria, David Chukwu (38) na Watanzania wawili katika  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu bado haujakamilika.

Mbali na Chukwu ambaye ni Mkazi wa Masaki, washitakiwa wengine ni Isso Lupembe (49) Mkazi wa Mbezi na Allistair Mbele (38).

Wakili wa Serikali, Ester Martin alidai jana mbele ya Hakimu Mfawidhi Godfrey Isaya kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi bado haujakamilika.

Hakimu Isaya aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 21, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Washitakiwa walikamatwa Aprili 15, mwaka 2020, wakiwa na dawa za kulevya aina ya heroin zinazokadiriwa kuwa ni zaidi ya kilogramu 270.

Katika tarehe hiyo washitakiwa wanadaiwa walikutwa  maeneo ya Mbezi Kibanda cha Mkaa wakisafirisha kilogram 268.50 za dawa za kulevya aina ya heroine.

Inadaiwa Januari Mosi 2016 na Aprili 15,2020 walijihusisha na miamala ya fedha Dola za Marekani 61,500 na Sh 17,835,000 huku wakijua ni zao tangulizi la biashara ya dawa za kulevya.

Washitakiwa hao  wanakabilika na makosa ambayo hayana dhamana.

No comments: