ULEGA AKABIDHI MAGODORO 70 KAMBI YA WATU WALIOPO KARANTINI MKURANGA
NA MWAMVUA MWINYI,MKURANGA
Mbunge wa Jimbo la Mkuranga na Naibu wa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amekabidhi Magodoro Sabini (70) kwa ajili ya kambi ya watu walioko kwenye karantini wilayani Mkuranga.
Hatua hiyo ya Ulega ni kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za serikali za kupambana na ugojwa wa Homa ya Mapafu unaosababishwa na virusi vya Corona ambao umekuwa janga la Ulimwengu.
Magodoro hayo, Mbunge huyo aliyapokea kutoka kwa wadau na marafiki mbalimbali walioamua kuunga mkono jitihada za serikali kupambana dhidi ya corona.
Akipokea magodoro hayo ,mkuu wa wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga alimshukuru Mbunge Ulega kwa jitihada hizo na amewaomba wadau mbalimbali kuendelea kuunga mkono juhudi hizi za serikali za kupambana dhidi ya corona.
No comments: