MHOLA WAKABIDHI MSAADA WA VIFAA KINGA DHIDI YA CORONA


Na Abdullatif Yunus Michuzi TV.

Shirika la lisilokuwa la Kiserikali linalojihusisha na utoaji wa msaada wa kisheria pamoja na malezi na makuzi ya watoto Wilayani Muleba limetoa vifaa vya kujikinga na ugonjwa wa Corona kwa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba, ikiwa ni harakati na muendelezo wa mapambano dhidi ya Corona.

Akikabidhi vifaa hivyo kwa Mkuu wa Wilaya ya Muleba pamoja na viongozi wengine wa Wilaya hiyo Mkurugenzi wa Shirika hilo Bwana Saulo Marauli amesema kuwa vifaa hivyo ni pamoja na Barakoa ,Gloves (Neogloves ), Vitakasa mikono, ndoo za maji tiririka pamoja na gharama za mafuta na posho za matangazo kwa jamii ambapo vifaa vyote vina thamani ya shilingi milioni 6,760,000.

Akizungumza mara baada ya kupokea vifaa hivyo Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhandisi Richard Ruyango ameshukuru Shirika hilo na kuwaomba wadau wengine wa maendeleo kuiga mfano huo ikiwa ni mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona. 

 Aidha kwa upande wake Mganga Mkuu Wilaya ya Muleba Dkt. Modest Rwakaemula amesema kuwa vifaa hivyo vitapelekwa katika vituo mbalimbali vya afya vilivyopo Wilayani humo ili kuwasaidia wahudumu wa afya, juu ya mapambano haya, na vingine vitapelekwa katika kituo kilichotengwa kwa ajili ya washukiwa (karantini).
Pichani Ni makabadhiano ya Vifaa kinga dhidi ya Corona vilivyotolewa na Shirika linalojihusisha na Masuala ya Kisheria lililopo Wilayani Muleba, wakati vifaa hivyo vikikabidhiwa kwa Mkuu wa Wilaya Muleba Mhandisi Richard   Ruyango.
 Picha ya Pamoja Mara baada ya Mkuu wa Wilaya Muleba Mhandisi Richard Ruyango kupokea Vifaa kinga kutoka MHOLA, tukio lililofanyika mapema Mei 04 katika Ofisi za Halmashauri Muleba.
 Pichani ni Muonekano wa baadhi ya Ndoo zilizokabidhiwa na MHOLA ikiwa ni sehemu ya Vifaa kinga vilivyotolewa na Shirika hilo kukabiliana na gonjwa la Corona Wilayani Muleba.

 

No comments: