AHSANTE SANA RAIS MAGUFULI

Na Emmanuel J. Shilatu

Ni gumzo gumzo gumzo kila kona. Si vijiweni, sokoni, maofisini, barabarani, majumbani, ama mitandaoni. Kote ni gumzo kufuatia hotuba aliyoitoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli wakati akimuapisha Dk. Mwigulu Nchemba kuwa Waziri mpya wa Katiba na Sheria.

Awali ya yote napenda kuungana na Mamilioni ya Watanzania kumpongeza Rais Magufuli kwa hotuba hiyo murua aliyoitoa iliyoibua gumzo kubwa ndani na nje ya nchi.

Watanzania walijawa na hofu kubwa wanapoona zimepostiwa picha za Watu wamefariki, wengine wakizikwa kutoka mitandaoni; mara wajuzi wakitueleza kila kifo ni Corona. Wanakuja kuamini ya mitandaoni kufuatia taarifa ya Kiserikali inayotoka kuonyesha idadi ya Wagonjwa ikiongezeka. Kumbe ongezeko lote hilo inawezekana ndani yake kuna walioongezwa tu kutokana na kutokuwepo kwa vipimo thabiti. Lakini Jana Rais Magufuli ulitutuliza mioyo yetu na kuanza kuamini tatizo sio kubwa na kuanza kupuuza habari za mitandaoni.

Hata WHO kupitia Mkurugenzi wake Mkuu Ndg. Tredos Ghebreyesu  walikiri vipimo vya wagonjwa wa COVID19 Afrika sio sahihi sababu ya vipimo sio thabiti! Asante Rais wa JMT Baba John Pombe Magufuli kwa kutuweka wazi juu ya hili. Hakika wewe ni Simba wa Afrika.

Ukazidi kuwaondoa hofu mpaka Watumishi wa Umma juu ya hatma ya uchumi wao ambao wengi walianza kuhisi waendapo hata mishahara watakosa lakini Jana uliwapa uhakika kuwa utaendelea kuwalipa mishahara mpaka na Waalimu wote ambao kwa sasa wapo likizo. 

Katika kuonyesha unasema kweli hata mshahara wa mwezi wa nne ulioisha uliwalipa mapema sana Watumishi wa Serikali hata wale waliopo likizo. Nchi nyingi zimeshindwa hili, lakini JPM Mwamba wa Afrika ameliweza hili. Nani kama JPM?

Ahsante sana Rais Magufuli kwa kutuondolea hofu, kutujaza matumaini mapya ya kiafya na ya  kiuchumi. Tunakuwahidi kuwa nawe bega kwa bega nyakati zote tukishikamana nawe katika kupambana na adui Covid 19 anayesababishwa na kirusi Corona. Tupo pamoja sana Baba yetu Dk. Magufuli.

Tanzania bila Corona inawezekana.
Jilinde; Nilinde; Tulindane
Wabheja sana!!

*Shilatu E.J*
0767488622

No comments: