FAROUK SHIKALO AITWA TIMU YA TAIFA KENYA

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Benchi la Ufundi la timu ya Kenya limetangaza kikosi cha wachezaji wake kitakachocheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Uganda kwa ajili ya kujiandaa na michezo ya kutafuta tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia  Qatar 2022.

Kenya atacheza mchezo wa kirafiki na Uganda wakati wa mapumziko ya kalenda ya michuano ya Kimataifa

Timu hizo hazina majukumu ya michezo ya awali kusaka nafasi ya kutinga makundi ya Afrika katika kutafuta tiketi ya kutinga fainali za kombe la dunia zitakazofanyika Qatar mwaka 2022

Wachezaji walioitwa ni pamoja Golikipa wa Yanga Faruk Shikalo , Patrick Matasi (St. George SC, Ethiopia ), John Oyemba (Kariobangi Sharks, Kenya),Timothy Odhiambo (Ulinzi ), Johnstone Omurwa (Wazito,Kenya), Brian Otieno (Bandari, Kenya) na David Owino (Mathare, Kenya)

Wengine ni Hillary Wandera (Tusker, Kenya), Dennis Odhiambo (KCB, Kenya),Lawrence Juma (Gor, Kenya), Nicholas Kipkirui (Gor Mahia, Kenya), Enosh Ochieng (Ulinzi, Kenya), Timothy Otieno (Tusker, Kenya),Michael Olunga (Kashiwa Reysol FC, Japan), Jesse Were (Zesco United, Zambia) na John Avire (Sofapaka, Kenya)

Kutoka ukanda wa Afrika Mashariki, Tanzania, Burundi na Rwanda zinakabiliwa na michezo hiyo

Tanzania itacheza na Burundi, mchezo wa kwanza ukitarajiwa kupigwa huko Burundi Septemba 02 na marudiano kufanyika uwanja wa Taifa Septemba 08

No comments: