Rollers Waingia Ubaridi, Waanza Visingizio
SHOO ya Yanga na Township Rollers kwenye marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika itapigwa jijini hapa Jumamosi saa 10:30 jioni lakini jamaa wameanza kuingiwa mchecheto.
Kwanza wamepunguza viingilio huku wakipigia magoti mashabiki wajazane kwa wingi kama Yanga walivyowafanyia Taifa kwenye sare ya bao 1-1. Kiingilio cha chini Jumamosi ni Buku 2 na cha juu buku kumi.
Winga wa Rollers Motsholetsi Sikele ambaye ndiye mashabiki wanamtegemea awavushe, amewapa
angalizo kwamba Yanga hii si ile ya kipindi kile na kwamba sapoti yao inahitajika kwa kiasi kikubwa kwa vile kazi bado ni ngumu.
Sikele ameliambia Spoti Xtra kwamba wanapata hofu ya kupata matokeo mazuri kwenye huo kutokana na ubora wa kikosi cha Yanga ambacho wamekuwa wakikifuatilia na kugundua kwamba kinazidi kubadilika. “Yanga si wale wakati ule, ni timu imara na yenye malengo.
Tunawaomba mashabiki wa Rollers wote kwa pamoja kujitokeza kwa wingi katika mchezo wetu
kama wale wa Yanga walivyojaa kwenye mechi ya kwanza.
“Tunahitaji sapoti yao itakayotuwezesha sisi kupata matokeo mazuri katika mchezo huu wa nyumbani, Yanga siyo nyepesi kama ilivyokuwa ya msimu uliopita ambayo tulikutana nayo mwaka 2018. Hii ya sasa ipo fiti na ina uwezo wa kupiga pasi hadi 20, hivyo tuna kibarua kigumu kuelekea mchezo huu,”alisema mchezaji huyo.
Wiki iliyopita kipa wao namba moja alidokeza kwamba anahofia sana guu la kushoto la Patrick Sibomana na analifanyia kazi ya ziada mazoezini
The post Rollers Waingia Ubaridi, Waanza Visingizio appeared first on Global Publishers.
No comments: