DIANA: KASHFA HAIWEZI KUNIBADILISHA
Mwigizaji wa filamu za Kibongo, Diana Kimari amefunguka kuwa siku zote habadiliki kwa kusimangwa kwa maneno na anaposemwa ndiyo kwanza anaendelea na mambo yake.
Akizungumza na Amani, Diana alisema kuwa watu wanajisahau mno na kufikiri kuwa ukimsema mtu kwa maneno makali na kashfa kama siyo za kweli hayawezi kumbadilisha hata kidogo.
“Niwakumbushe watu tu kuwa mimi ni yuleyule, sibadiliki hata kidogo na maneno hayanifanyi kuwa Diana wa tofauti yaani haiwezi kutokea, naendelea na mambo yangu kama kawaida,” alisema Diana bila kutaja anatafunywa na kashfa gani.
Hivi karibuni Diana alidaiwa kupewa kichapo na mama wa mwigizaji Wema Sepetu, Miriam Sepetu baada ya bi mkubwa huyo kudai hafurahishwi na tabia za mrembo huyo.
Stori: IMELDA MTEMA
The post DIANA: KASHFA HAIWEZI KUNIBADILISHA appeared first on Global Publishers.
No comments: