SAKATA LA KAKOLANYA NA YANGA LAPELEKWA MAHALA PENGINE
Unaambiwa lile sakata la mchezaji wa Yanga, mlinda mlango Beno Kakolanya limezidi kuchukua taswira mpya baada ya mwanasheria wake, Leonard Richard kufikisha suala lake kunako Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Mwanasheria huyo ameamua kufikia maamuzi hayo ili kupata suluhisho sahihi baada ya kuona hakuna dalili za kufanikiwa kwa kuzungumza na upande wa mwajiri ambaye ni Yanga pekee.
Taarifa zinasema mwanasheria Richard amekuwa akizungushana na Yanga bila kufikia mwafaka kama ambavyo walikubaliana na mwisho wa siku imebidi awasili TFF.
Ikumbukwe sakata hili lilianza tangu Kakolanya agome kujiunga na timu iliposafiri kuelekea kanda ya ziwa kwa madai ya stahiki zake ikiwemo fedha za mshahara.
Mpaka sasa Kakolanya amekuwa akifanya mazoezi binafsi bila kuwa na timu yoyote ya kuchezea huku Ligi Kuu Bara ikiwa katika mzunguko wa pili.
The post SAKATA LA KAKOLANYA NA YANGA LAPELEKWA MAHALA PENGINE appeared first on Global Publishers.
No comments: