Matibabu ya Ruge ni Tsh 5m kwa Siku, Familia Yaomba Sapoti!
FAMILIA ya Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba wamesema gharama za matibabu ya ndugu yao huyo ambaye anatibiwa nchini Afrika Kusini ni kubwa sana, hivyo wameomba msaada wa fedha kwa ajili ya kusaidia kulipia gharama za matibabu hayo.
Akizungumza katika mahojiano na Televisheni cha Clouds jana Jumatatu, Februari 18, mdogo wa Ruge aitwaye Mbaki Mutahaba alisema kwa sasa Ruge anapatiwa matibabu Afrika Kusini ambako kwa siku gharama ni Sh milioni 5 hadi Tsh milioni 6.
“Ruge alianza kuugua mwaka 2018, alilazwa katika Hospitali ya Kairuki kisha akapelekwa India, ana figo ambayo haipo sawasawa ilikuwa lazima wambadilishe. Madaktari wa hospitali ya Kairuki na Muhimbili wakashauri apelekwe Afrika Kusini maana ni karibu zaidi lakini gharama ni kubwa.
“Tunashukuru sapoti ni kubwa, hata Rais John Magufuli ametoa mchango na anaendelea na wengine wameendelea kuchangia, lakini gharama hizo ni kubwa kuliko kawaida. Afrika Kusini mfumo wao wa malipo ni tofauti unapaswa kulipa fedha taslimu.
“Kuna namba rasmi imeandikishwa kwa jina la mdogo wetu Kemilembe Mutahaba unaweza kutusaidia, kutuma ujumbe wa pole, faraja na hata wengine ambao wangetamani kutuma chochote, namba hiyo ni 0752222210,” alisema Mbaki.
DADA Amlilia DIAMOND “Msamehe Baba Kwani Tatizo Nini?”
The post Matibabu ya Ruge ni Tsh 5m kwa Siku, Familia Yaomba Sapoti! appeared first on Global Publishers.
No comments: