POLISI, MWALIMU WAIBUKA WASHINDI CHEMSHA BONGO NA UWAZI

Mhariri wa Global, Endrew Carlos (kushoto) akimkabidhi Afande Vincent Laurent shilingi 50,000 baada ya kuibuka mshindi.

POLISI wa Kituo Kikuu cha Kati (Sentro),Vincent Laurent na mwalimu wa Shule ya Keko-Magurumbasi, Jacqueline Mbawala wamejishindia kila mmoja kiasi cha shilingi 50,000 baada ya kushinda chemsha bongo inayoendeshwa na Gazeti la Uwazi. Akizungumza na mtandao huu, Jacqueline alisema mwanzoni alipopigiwa simu kuwa ameshinda majirani walimwambia huenda anatapeliwa lakini alipofika katika Ofisi za Global Group, Sinza-Mori jijini Dar ndipo akaamini kuwa ni kweli.

Mhariri wa Global, Endrew Carlos (kushoto) akimkabidhi mwalimu Jacqueline Mbawala shilingi 50,000 baada ya kuibuka mshindi

“Yaani wakati napokea simu naambiwa kuwa nimeshinda, waliniambia haiwezekani kushinda lakini nikajipa nguvu na kufika hapa (Global). Nashukuru kwa kweli mnatoa zawadi na niwaombe wengine ambao hamshiriki mjaribu bahati hii,” alisema Jacqueline.

Mwalimu Jacqueline Mbawala akifurahia kitita chake cha shilingi 50,000

Kwa upande wa Vincent alisema amekuwa akishiriki bahati nasibu nyingi lakini hakuwahi kukata tamaa. “Nilishiriki ile ya nyumba mshindi akatokea Iringa, ilipokuja nyingine nikasema siwezi kukosa napo bahati haikuwa yangu. Kifupi sikuwa mtu wa kukata tamaa, kila chemsha bongo hizi na bahati nasibu zilizokuwa zinatoka lazima nishiriki hadi hii ya mwisho nikapigiwa simu na kuambiwa nimeshinda.

Mwalimu Jacqueline Mbawala na Afande Vincent Laurent wakifurahia mikwanja yao

“Nawaombeni wengine ambao mnashiriki hili jambo ni la kweli kabisa na pesa unapewa ‘cash’ hakuna longolongo,” alisema Vincent. Wengine walioshinda hadi sasa ni Masoud Kinyogoli wa Kitunda jijini Dar, Sabati Maghamba wa Same, Mohammed Elly wa Morogoro na Hamis Mohammed wa Magomeni ambapo wote walijishindia shilingi 50,000 na mmoja, Maneno Masika wa Mbagala akiondoka na simu janja ya kisasa.

Stori: Mwandishi Wetu

The post POLISI, MWALIMU WAIBUKA WASHINDI CHEMSHA BONGO NA UWAZI appeared first on Global Publishers.

No comments: