‘BETIKA’ LAZIDI KUTIKISA MTAANI, KILA KONA LINAGOMBEWA!
GAZETI namba moja na la kijanja linalohusu ishu nzima za kubeti lijulikanalo kwa jina la BETIKA ambalo linatolewa bure, leo Jumatano limeingia mtaani kwa mara ya pili.
Kila Jumatano, gazeti hilo linaingia mtaani na linagawiwa bure kwa watu wenye umri kuanzia miaka 18. Mara baada ya toleo la kwanza kutoka, wadau mbalimbali walilipokea vizuri na kulimwagia sifa kemkem.
Mapema leo, timu nzima ya maofisa Masoko wa Kampuni ya Global Publishers ambayo ndiyo inachapisha gazeti hilo, imetinga mtaani kwa ajili ya kulinadi gazeti hilo.
Mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam kuanzia Kituo cha Daladala cha Simu 200, Ubungo Stendi ya Mkoa, Manzese na maeneo mengine, timu ya usambazaji ilipita huko kote na kuligawa gazeti hilo lenye maujanja mengi ya kubeti.
Ofisa Masoko wa Global Publishers, Mussa Mgema, alisema kuwa mapokeo ya gazeti hilo yamekuwa makubwa, hali inayodhihirisha kwamba wasomaji hasa wazee wa kubeti walikuwa na kiu kubwa ya bidhaa kama hiyo.
“Gazeti hili ni mahsusi kwa ajili ya ishu nzima ya kubeti, lina makala nyingi zinazoelezea kampuni mbalimbali za kubeti, lakini pia humo ndani kuna odds zinazomfanya msomaji kupata njia rahisi za kubeti.
“Tangu liingie mtaani wiki iliyopita, tumepata mrejesho mzuri kwamba wasomaji wanalihitaji sana, hivyo katika toleo hili la pili, tumeamua kuongeza kopi ili kuwafikia wasomaji wetu wengi na kukata kiu yao,” alisema Mgema.
Gazeti hilo lenye kurasa 20 ambazo zote ni za rangi, mbali na kuwa na makala na odds za kampuni mbalimbali, pia kuna takwimu za ligi kubwa barani Ulaya.
MWANDISHI WETU
The post ‘BETIKA’ LAZIDI KUTIKISA MTAANI, KILA KONA LINAGOMBEWA! appeared first on Global Publishers.
No comments: