Babu Mlemavu Ateketea kwa Moto Aliowasha Shambani Kwake
MKAZI wa kijiji cha Kilongo, Muheza mkoani Tanga, Saidi Sekizenge (72), amefariki dunia kwa kuteketea kwa moto akiwa shambani kwake. Tukio hilo lilitokea juzi katika kijiji hicho ambako Sekizenge alikuwa anaishi na familia yake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Edward Bukombe, alisema mzee huyo alifariki dunia kutokana na kuungua na kuteketea wakati akichoma moto majani yaliyokuwa yamekauka shambani mwake.
Alisema wakati akichoma majani hayo shambani, ghafla moto ulimzidi nguvu kutokana na upepo mkali, hivyo kuhamia katika mashamba ya jilani ambayo wamepakana na shamba lake na moto kuanza kuyaunguza.
Kamanda Bukombe alisema baada ya moto huo kusambaa katika shamba ya hayo, Shekizenge alijaribu kuuzima ili lakini alizidiwa na moshi wa moto na kuzingirwa na moto, kushindwa kukimbia kutokana na ulemavu aliokuwa nao na hatimaye kuungua mpaka kuteketea kabisa.
Diwani wa Songa wilayani Muheza, Leslie Nchimbi, alisema baada ya tukio hilo, viongozi walitoa taarifa katika kituo cha Polisi Wilaya ya Muheza. Alisema polisi na daktari kutoka Hospitali Teule ya Wilaya ya Muheza, walifika eneo la tukio kwa ajili ya uchunguzi kisha kuruhusu mwili wake uzikwe baada ya uchunguzi.
CREDIT: NIPASHE
The post Babu Mlemavu Ateketea kwa Moto Aliowasha Shambani Kwake appeared first on Global Publishers.
No comments: