Okwi, Kagere Wawaingiza Chaka Mashabiki Arusha

Emmanuel Okwi

MASTAA wawili wa Simba, Emmanuel Okwi na Meddie Kagere waliwaingiza chaka mashabiki wa timu hiyo ambao walifika jana mkoani Arusha kwa ajili ya kuwatazama wachezaji hao wakiwa na kikosi hicho.

 

Simba jana Jumanne walikuwa ugenini mkoani hapa kwa ajili ya pambano lao la Ligi Kuu Bara dhidi ya African Lyon lililopigwa katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Mashabiki kutoka sehemu mbalimbali za mkoani hapa walifika uwanjani ikiwa ni maalum kwa ajili ya kuwaona mastaa hao ambao waliongoza mauaji dhidi ya Yanga wiki moja iliyopita lakini waliambulia patupu kutokana na kutowaona.

 

Okwi na Kagere hawakuwa sehemu ya kikosi cha Simba ambacho kilitua mkoani hapa kutokana na kubakishwa Dar.

Wachezaji hao wanakabiliwa na adhabu ya kuwa na kadi tatu ambazo ziliwafanya walikose pambano hilo. Wachezaji hao watakuwa huru kucheza mechi ya Ijumaa dhidi ya Azam FC.

Stori na Sweetbert Lukonge

The post Okwi, Kagere Wawaingiza Chaka Mashabiki Arusha appeared first on Global Publishers.

No comments: