BETIKA: Asanteni sana kwa kutupokea vizuri
HILI ni toleo la pili la gazeti hili la Betika, ambalo ni mahususi kwa ajili ya matangazo na taarifa zinazohusiana na michezo ya kubahatisha – betting na lotto.
Toleo letu la kwanza lilikuwa wiki iliyopita. Vijana wetu walisambaa kila kona ya Jiji la Dar es Salaam kugawa gazeti hili bure. Katika Uwanja wa Taifa wa Dar es Salaam wakati wa mechi ya Simba na Yanga, vijana wetu walikuwa wakigawa gazeti hili uwanjani hapo.
Aidha, kupitia mawakala wetu wa mikoa mbalimbali Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar, gazeti hili limesambazwa kwa kasi. Sisi Betika tunawashukuru kwa kutupokea na hasa kwa wale ambao wametuma maoni yao kupitia namba zetu.
Tunawaahidi tutaendelea kuwapa habari za ushuhuda wa washindi wa michezo mbalimbali ya kubahatisha, misimamo ya ligi mbalimbali za Ulaya na wachambuzi wakali ambao watakusaidia namna ya kubashiri kwa ushindi.
Mwisho, tunaendelea kuwakaribisha watangazaji wote kutangaza nasi. Ni gazeti linalosambazwa nchi nzima na kuwafikia walengwa. Endelea kuburudika na Betika.
The post BETIKA: Asanteni sana kwa kutupokea vizuri appeared first on Global Publishers.
No comments: