Gazeti la Betika Limekomboa Matangazo ya Kubeti

Siku chache baada ya serikali ya Tanzania kutangaza kusitisha kwa muda matangazo ya michezo ya bahati nasibu na kubashiri matokeo kwenye redio na runinga, mkombozi mpya wa matangazo hayo amepatikana.

 

Mkombozi huyo ambaye pia ndiye habari iliyopo mjini ni Gazeti la Betika.

Unachotakiwa kufanya ni kitu rahisi tu, ingia mtaani utafute nakala ya Gazeti la Betika, hilo gazeti ni bure kabisa.

Nenda sehemu kunapouzwa magazeti kila Jumatano umwambie muuzaji akupe Betika lako, au ukifika wewe jichukulie tu usepe zako wala hawezi kukuambia lolote.

Humo ndani ya Gazeti la Betika kuna kila kitu kitakachokurahisishia mambo ya kubeti na umgaragaze ‘mdosi’.

Ukiwa na Betika wewe ndiye mjanja wao, kila siku utakuwa unajipigia tu kwenye kubeti.

 

Nakala ya kwanza la Betika ilitoka Jumatano iliyopita na kung’ang’aniwa kwelikweli jambo ambalo uongozi wa gazeti hilo umeahidi kwamba wiki hii utaongeza oda kubwa ili lifike kwenye vijijini vingi zaidi.

 

Gazeti hilo pekee nchini ambalo litakuwa linakuhabarisha kuhusiana na mambo ya kubeti na wapi unapopaswa kuweka mkeka wako, wataalam kibao wa mambo ya kubeti wamekurahisishia kazi ndani ya Betika.

Mara baada ya toleo hilo la kwanza kutoka, wafanyakazi wa Global Publishers ambao ndiyo wachapishaji wa gazeti hilo, walipiga nalo picha mbalimbali wakiwa kwenye nyuso za furaha kuashiria bidhaa yao ni bora.

 

Akizungumzia ujio wa gazeti hilo, Kezilahabi Peresi ambaye ni Ofisa Masoko wa Gazeti la Betika, alisema ndani ya Betika wasomaji watapata makala kali za burudani na michezo bila kusahau hadithi ya kusisimua.

 

“Zaidi ya habari na uchambuzi wa mechi mbalimbali za ligi za nje, gazeti hili litakuwa linakuletea matangazo kutoka katika kampuni zinazoendesha michezo ya kubahatisha.

“Sisi Betika tunaamini, gazeti letu ni fursa nzuri kwa wabetiji wote kuelewa kwa undani kuhusiana na michezo ya kubahatisha, mambo ya kuzingatia ili kubeti kwa mafanikio na kuvuna fedha kwa wingi,” alisema Peresi na kuongeza:

“Tumetenga sehemu maalumu kwa ajili ya kuweka mikeka ya kubeti kutoka katika kampuni mbalimbali. Betika litakusaidia kuwa mbetiji wa faida badala ya kuwa msindikizaji.

 

“Betika ni tofauti na magazeti mengine, gazeti letu haliuzwi, utalipata bure kabisa. Kwa msingi huo, ukikutana na gazeti hili mahali popote, usikubali kutoa fedha yako, utatakiwa kuchukua bure.

 

“Timu nzima ya Betika tunawahakikishia tumejipanga vilivyo kukuhabarisha na kukupa mbinu za kuwa mbetiji bora, lakini milango ipo wazi kutoa maoni yako kwa lengo la kuboresha zaidi.

 

“Hatutasita kupokea maoni na kuyafanyia kazi, yale yaliyo bora na yenye tija. Jione sehemu ya Betika kwa kututumia maoni yako kupitia mawasiliano yetu yaliyomo ndani ya gazeti hilo.

 

“Wanaohitaji kutangaza nasi tunapatikana kupitia namba 0755826488 na 0659472001 au kupitia barua pepe betika255@ gmail.com.”

The post Gazeti la Betika Limekomboa Matangazo ya Kubeti appeared first on Global Publishers.

No comments: