Zahera: Tunaweka Rekodi Mpya Mwanza Leo
KOCHA wa Yanga, Mwinyi Zahera, amefunguka kuwa, wachezaji wake hawatakiwi kuwa na akili ya kuwaza wanaenda kufungwa kwa sababu kila jambo lina mwanzo na mwisho wake.
Leo Jumatano, Mbao inacheza na Yanga kwenye Uwanja wa CCM Kirumba uliopo
jijini Mwanza ukiwa muendelezo wa mechi za Ligi Kuu Bara.
Yanga imeshindwa kutamba katika uwanja huo ukiwa ni msimu wa tatu haijapata ushindi.
Akizungumza na Championi Jumatano, Zahera alisema; “Nimewaambia wachezaji wangu kuwa kila kitu kina mwanzo na mwisho, hivyo ni lazima tufute historia na kuona timu yetu inafanikiwa kupata matokeo mbele ya Mbao FC tofauti na huko nyuma.” “Morali ya wachezaji ipo juu na malengo ni kuona wanafanya vizuri kwa kucheza kwa nidhamu na ufundi kama ilivyokuwa kwenye mechi yetu na Simba.
“Na pia nimeambiwa Yanga na Simba wamekuwa wakipata shida kwenye uwanja huu lakini nimejipanga
kutengeneza historia mpya,” alisema Zahera.
Yanga msimu huu imepoteza mechi mbili dhidi ya Stand United na Simba lakini bado ipo kileleni kwa pointi 58.
Stori na Martha Mboma
The post Zahera: Tunaweka Rekodi Mpya Mwanza Leo appeared first on Global Publishers.
No comments: