Walivyokuwa wakiisikia Pemba kwa uovu, wabaini tofauti

Walivyokuwa wakiisikia Pemba kwa uovu , wabaini tofauti na ilivyokua ikitangazwa September 1, 2018 – by Manager Imeandikwa na Salmin Juma , Pemba Wananchi kiswani Pemba na Zanzibar kwa ujumla, wametakiwa kuwa makini hakikisha amani inazidi kutawala nchini ili hatua za kimaendeleo ziweze kufikiwa na kila mmoja aisha kwa furaha na amani. Wito huo ulitolewa jana na Katibu tawala mkoa wa kusini Pemba Mh Yussuf Mohd Ali kwa niyaba ya Mh Mkuu wa mkoa huo Hemed Suleiman aliyemuwakisha katika sherehe za kuwaaga wanajamuia ya UVIKIUTA ambao walipiga kambi kwa wiki moja eneo la vitongoji Kusini Pemba. UVIKIUTA ni jumuiya ambayo imejitolea kuja Pemba kufanya kazi za kujitolea kama vile kufanya usafi wa kimazingira, ikiwamo kupanda miti ya mikoko baharini, pamoja na kupaka rangi katika majengo mbalimbali. Mh Hemed kupitia katibu tawala huyo alisema wanafarijika sana kusikia kuwa moja miongoni mwa malengo ya ujio huo ni kudumisha amani, amesema jambo hilo ni kubwa kwani ndilo linaloleta maendeleo “ tumefarijika sana kusikia kuwa ujio wenu pia upo kwaajili ya kudumisha amani , kwakweli hili ni jambo zuri linalopaswa kudumishwa”alisema katibu tawala huyo. Mmoja miongoni mwa wanajumuia hiyo Mr Julian Ferrage alisema “tunafahamu namna gani maji yanavyosogea baharini kuja juu, hivyo tuliamua kupanda mikoko ili kuhifadhi mazingira kwani miti hiyo inasaidia sana , kwahiyo safari yetu imekua na manufaa kwani tumefanikiwa kupanda miti hiyo katika bahari. Akielezea walichojifunza tokea fika kisiwani Pemba Mwenyeki wa UVIKIUTA Mr Ben Mongi , aalisema baadhi ya vyombo vya habari vimekua vikiisema vibaya Pemba kua ni sehemu ya machafuko na vurugu wakati hali haiku hivyo. “ tulipokua hatujaja tulikua tunasikia kupitia vyombo vya habari kuwa , pemba ni sehemu ya vurugu, na hakuna amani kumbe sivyokabisa , watu wapemba ni wapenda amani na watulivu”alisema Mr Ben. Jumala ya vijana 75 kutoka mataifa 11 duniani kama vile , Japan, Kenya , France, Maxco, Ujerumani wamekuja kisiwani Pemba , kwa lengo la kushiriki kazi tofauti ikiwamo kupanda miti, kupaka rangi majengo na shuhuli zote za utunzaji wa mazingira.. pembatoday

The post Walivyokuwa wakiisikia Pemba kwa uovu, wabaini tofauti appeared first on Mzalendo.net.

No comments: