Maalim Seif akutana na madiwani Dar

Na Anderson Ndambo Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad Amekutana na madiwani wa CUF Mkoa wa Dar es salaam, na kuzungumza nao masuala mbalimbali juu ya mustakabali wa CUF na Taifa kwa ujumla. Ametumia pia nafasi hiyo kuwaimarisha madiwani hao, pamoja na kuweka bayana namna ccm na serikali yake kupitia kwa kiongozi wao, namna alivyokusudia kuuwa demokrasia nchini, kwa kuviua vyama vya upinzani. Ameendelea kuwasihi madiwani kuwa waaminifu kwa watu waliowapa dhamana na wathamini heshima waliopewa na wananchi kupitia chama cha CUF. Aidha, ametolea ufafanuzi juu ya biashara haramu ya kuwanunua baadhi ya wapinzani, ili kuv7hakq vyama hivi, kwamba wako waliofanikiwa kuwapata lkn wapo ambao ccm imeshindwa kuwanunua kutokana na msimamo wao mkali na dhamira zao za kuendelea kukisimamia na kukipigania kile wanacho kiamini. Pia ameendelea kuwashukuru madiwani hawa kwa uthabiti wao na msimamo wao, pamoja na vitisho na majaribio ya kuwanunua kuwa mengi sana. A. Ndambo

The post Maalim Seif akutana na madiwani Dar appeared first on Mzalendo.net.

No comments: