JIONI YA BARAKA FAMILIA YA OYA YASHIRIKI IFTAR NA JAMII

 Taasisi ya Oya Micro-crediti imeandaa futari maalum kwa wateja wake na jamii kwa ujumla tukio lililolenga kuimarisha mshikamano wa kijamii.

Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ni wakati wa kutafakari, kushukuru, na kushirikiana na jamii katika kujitoa kwenye mambo mablimbali. Kwetu OYA, tunaamini kuwa mafanikio ya kweli hayapimwi tu kwa ukuaji wa biashara, bali pia kwa mchango chanya tunaoutoa kwa jamii inayotuzunguka.

Oya Micro-crediti tulipata heshima ya kuandaa Iftar dinner maalum iliyowaleta pamoja watumishi wetu, baadhi ya wateja na wageni maalum katika mazingira ya mshikamano na furaha.

Moja ya sehemu iliyogusa mioyo ya wengi ilikuwa uwepo wa watoto wazuri kutoka kituo cha kulelea watoto yatima kilichopo Kinondoni watoto hao walionesha Tabasamu lao lililota furaha kubwa na kutukumbusha maana halisi ya  ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan — huruma, upendo, na kushirikiana.

Haikua tu hafla ya kufuturu pamoja, bali pia ya kuimarisha mahusiano, kujenga mshikamano wa kijamii, na kueneza matumaini matukio kama haya yanatukumbusha kuwa hata matendo madogo ya wema yanaweza kuleta furaha kubwa kwa wengine.

Tunatoa shukrani zetu za dhati kwa kila mmoja aliyeshiriki na kuchangia kufanya siku hii iwe ya kipekee kadri mwezi wa Ramadhan unavyoendelea, OYA itaendelea kujitahidi kushirikiana na jamii na kuendeleza maadili ya umoja, huruma, na kusaidiana.

Kwa niaba ya familia nzima ya OYA, tunawatakia wote Ramadhan yenye baraka na amani. Alisema Mkurugenzi wa OYA Bwana. Alpha Peter




Ramadan Kareem. 🌙

No comments: