DK. SAMIA TUNAKUPENDA NA TUTAKUCHAGUA

 


Na Said Mwishehe,Michuzi TV

JUZI kati nilikuwa na mshikaji wangu fulani hivi basi tukawa tunapiga stori kuhusu nchi yetu chini ya uongozi wa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan

Katika mazungumzo yetu tukakubaliana kwa kauli moja Rais Dk.Samia tunampenda na katika uchaguzi mwaka huu tutamchagua tena kiroho safi.Tunampenda naye anatupenda.

Zipo sababu nyingi za kumchagua Rais Samia katika uchaguzi mkuu mwaka 2025.Ukweli hatuna shaka naye na kwa sasa tunatamba naye.

Kabla ya kueleza baadhi ya sababu ambazo zinanifanya mimi na Watanzania wenzangu kumchagua Rais Samia katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 nitumie pia nafasi hii kuipongeza CCM kupitia Mkutano Mkuu maalum uliofanyika Januari 18 na 19 mwaka huu kupitisha azimio.

Katika azimio hilo limeweka wazi kuwa mgombea wao wa nafasi ya urais kwa tiketi ya Chama hicho ni Rais Dk.Samia Suluhu Hassan na Mgombea Mwenza ni Dk.Emmanuel Nchimbi ambaye kwa sasa ni Katibu Mkuu wa Chama hicho.

Hongereni CCM kwani azimio lenu ndio azimio letu, mawazo yenu ndio mawazo yetu,matarajio yenu ndio matarajio yetu.Yaani kwa lugha ya mjini tunasema 2025 Samia mitano tena,ndio eeeeh kama inakuuma sema.

Kwa jinsi ambavyo Rais Samia anaongoza nchi yetu tunaona kabisa nchi imetulia, iko tulivu na hakuna anayeishi kwa hofu,tunajivunua uongozi wa Rais Samia.

Wakati anakabidhiwa Nchi wapo waliodhani hataweza, hatafanya lolote hata miradi ya kimkakati haitakamilika lakini hivi sasa sote ni mashahidi Rais Samia ameweza na mambo yanakwenda, tunaraha wenyewe,hongera Rais Samia,tunakupenda na tutakuchagua.

Chini ya uongozi wa Rais Dk.Samia watanzania tunashuhudia utekelezaji wa miradi ya kimkakati iliyopo katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu,mambo ni moto,mambo ni faya.Miradi mingi imekamilika na mingine iko hatua za mwishoni.

Reli ya SGR leo ni mwendo wa kuteleza tu, unalala Dar na chai unakunywa Dodoma. Ukiondoka saa 12 kamili asubuhi Dar basi Dodoma utafika kwenye saa 3:42 au 3:45 kama hakutakuwa na changamoto.

Chini ya Rais Samia amehakikisha SGR ujenzi wake unaendelea na ujenzi wa reli hiyo umefika Makutupola na kazi inaendelea kuelekea Mwanza,Tabora pamoja na Kigoma.Mama Samia yupo kazini kwa kifupi kazi inaendelea.

Katika mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere kule Rufiji mitambo imewashwa na Watanzania tumeanza kujibweda,mgao wa umeme umekwisha na kama kunakuwa na mgao basi ni ule unaotokana na uchakavu wa miundombinu ambayo nayo uboreshaji wake unaendelea.Hongera Rais Samia tunakupenda na tutakuchagua.

Ujenzi daraja la Kigongo-Busisi katika Ziwa Victoria mambo safi , kazi ya ujenzi iko mwishoni na muda si mrefu tutashuhudia magari yakipita.Kwa wanaofuatilia wanajua wakati Rais Samia anaingia madarakani ujenzi ulikuwa umefikia hatua gani?Wakati Rais Samia anachukua Nchi daraja hilo ndio kwanza nguzo zilikuwa zimeaanza kuwekwa lakini leo hii ujenzi zaidi ya asilimia 95.

Kwa ambaye haamini ninachoeleza basi anayo nafasi ya kufunga safari aende kuangalia maana wengine wako kama Tomaso hawaamini mpaka waone.

Kwa kazi ambayo Rais Samia hakika tutalipa fadhila na shukrani zetu katika boksi la kura.Ametuheshimisha Watanzania na sisi tutamheshimisha kwa kumpigia kura.

Nafahamu kura ni siri ya mpigakura lakini kwa Samia wala hakuna siri kura yangu ni ya kwake na kura za Watanzania zote ni kwa Samia.

Kwa aliyofanya Samia kazi yetu ni kumpigania,kumtetea na kumuombea afya na uzima .Ikifika siku ya kupiga kura basi tukampigie kura.

Wakati natafakari yaliyofanywa na Rais Samia nimekumbuka jinsi ambavyo amefanikiwa kutibu ugonjwa wa miaka mingi wa uhaba wa madarasa hasa kwa shule za sekondari.

Kwa miaka mingi ilikuwa kila mwaka lazima wanafunzi wanaokwenda kidato cha kwanza wasubirie ujenzi wa madarasa ndio waende sekondari.Wakurugenzi na wakuu wa mikoa walikuwa wananyimwa likizo kisa wasimamie ujenzi.

Chini ya Rais Dk.Samia wanafunzi wote wanaotakiwa kujiunga na elimu ya sekondari wanaanza masomo siku moja kwa tarehe husika ambayo shule itafunguliwa.Katika hili Rais Samia anastahili pongezi.

Kwa upande wa huduma za maji Rais Samia kupitia Serikali anayoiongoza imeendelea kutatua changamoto ya uhaba wa maji safi na salama.Kupitia RUWASA ambao wanahusika na kusambaza maji vijijini wanaendelea na kazi ya kusambaza maji.

Kuna vijiji ambavyo tangu nchi ipate huru havikuwahi kupata maji safi na salama katika bomba lakini chini ya Rais Samia leo wananchi wanapata maji.Tunaposema Rais Samia tunampenda kwasababu yeye mwenyewe anaupendo mkubwa kwetu.

Rais Samia tangu ameingia madarakani ameendelea kutafuta ufumbuzi wa changamoto hatua kwa hatua na hili tunajivunia Watanzania.

Huduma za afya zimeendelea kuboreshwa na sasa dawa na vifaa tiba vya kisasa viko kuanzia zahati mpaka hospitali za rufaa.

Katika miundombinu ya barabara tunaendelea kushuhudia kazi inayofanywa na Rais Samia.Barabara zinaendelea kujengwa kila mahali na kwa Dar ea Salaam ujenzi barabara ya mwendo kasi kazi inaendelea na wakandarasi wako saiti.

Kauli mbiu ya Rais Samia inasema Kazi iendelee na kweli kazi inaendelea.Kama huamini kawaulize wa kulima.Ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji unaendelea kila mahali,Rais ametoa mabilioni ya fedha kutekelezwa kwa miradi.

Hapo sijazungumzia upatikanaji wa pembejeo za kilimo.Hakuna yale malalamiko mbegu imechelewa,mbolea haijafika.

Kwa kazi ambayo Rais wetu Dk.Samia ameendelea kuifanya na kuonekana zawadi pekee ambayo anastahili kupewa ni kushinda kwa kishindo.Sina mashaka hata kidogo ushindi ni kwa Dk.Samia

Lakini tuwe wa kweli katika uongozi wa Rais Samia ameendelea kusimamia haki za watu, uhuru wa kujieleza na kutoa maoni.Rais Samia ameponyesha majeraha kwa baadhi ya watu.Vilio vimepungua kikubwa kila mmoja afanye shughuli zake kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa.

Utulivu katika shughuli mbalimbali zikiwemo za kiuchumi zimesababisha hata mapato ya kodi kupaa.Nchi iko vizuri katika makusanyo ya kodi na Rais anasisitiza watu kuendelea kulipa kodi kwa inavyostahili.Asidhulumiwe mwananchi, wala Serikali isidhurumiwe.

Kabla ya kuhitimisha nimekumbuka dhamira njema ya Rais Samia katika kuboresha bandari zetu ikiwemo ya Dar es Salaam ambapo kuna baadhi ya watu walipinga uwekezaji wa DP World.Leo hii bandari ya Dar es Salaam hakuna tena msongamano wa meli bandarini, meli inakuja inashusha kontena na kuondoka.

Tafsiri kubwa katika uwekezaji wa bandari Rais Samia aliona mbali,alitazama maslahi mapana ya Nchi yake na leo tumeanza kuvuna matunda ya uwekezaji uliofanyika.Hongera Rais Samia,tunakupenda,tutakuchagua .Yaani mitano tena kwako Rais wetu.


No comments: