WASOMI ELIMU YA JUU 'TAHLISO' WAIJIA JUU CHADEMA | NI KWA KUIPINGA RIPOTI YA KIKOSI KAZI

Jumuiya ya Wanafunzi  Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO)  wamekionya Chama cha Demokrasia na Mendeleo (Chadema) Kutokana na tabia yake ya kupinga mambo mbali mbali yanayofanywa na Serikali hata kama yana manufaa kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.

Rais wa Jumuiya hiyo Frank Nkinda ametoa matamshi ya kukionya  Chama hicho Leo Jijini Dar es Salaam katika mkutano wake na Waandishi wa habari.

"Kwa kipindi kirefu, Chama hicho kimejijengea tabia ya  kutafuta uungwaji mkono hata katika masuala yasiyo na maslahi kwa Taifa na kupinga mapendekezo yenye dhamira  ya kuwaweka watanzania pamoja" amesema Nkinda

Akitolea mfano wa baadhi ya mambo hayo ikiwemo ripoti ya kikosi kazi iliyokabidhiwa  juzi kwa Rais Samia Suluhu Hassan ikiwa imesheheni mapendekezo mbali mbali yenye tija kwa taifa, Nkinda amesema wao kama wasomi wa Elimu ya juu hawaoni sababu yeyote ya Chadema kuendelea kuipinga ripoti hiyo. 

“Sote tulisikia muhtasari wa kile kilichowasilishwa na Mwenyekiti wa Kikosi kazi, Prof. Rwekaza Mukandala kwa Mhe. Rais, kwakweli dhamira yake ni njema. Sasa tumeshangaa Chama hicho cha Siasa kimekuja juu na kusema mapendekezo haya hayafai na kwamba ni matumizi mabaya ya fedha za umma, lakini ikumbukwe kwamba watu hawa waliitwa kutoa maoni yao wakakataa, sasa wanataka hata yale yaliyotolewa na  watanzania wengine kwa uhuru na haki watu wayapinge ”amebainisha  Nkinda 

Ameongeza kuwa TAHLISO kama Taasisi inayolea nguvu kazi ya Taifa, kimsingi wana mamlaka ya Kuonya, kukemea na kushauri mambo mbalimbali katika Kuchochea maendeleo ya Taifa.





No comments: