BENKI YA NBC ILIVYOIPAMBA DERBY YA KARIAKOO

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambae ni mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara, NBC Premiere League Bw Theobald Sabi (Kulia) akikabidhi tuzo kwa mchezaji wa klabu ya Yanga Feisal Salum alietangazwa mchezaji bora wa ligi hiyo kwa mwezi Septemba wakati wa mechi kati ya Yanga na Simba iliyofanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam jana. Timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambae ni mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara, NBC Premiere League Bw Theobald Sabi (Kulia) akikabidhi hundi yenye thamani ya sh mil 1 kwa mchezaji wa klabu ya Yanga Feisal Salum alietangazwa mchezaji bora wa ligi hiyo kwa mwezi Septemba wakati wa mechi kati ya Yanga na Simba iliyofanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam jana. Timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambae ni mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara, NBC Premiere League Bw Theobald Sabi (Kushoto) akisalimiana na wapenzi wa mchezo wa huo wakati wa mechi kati ya Yanga na Simba iliyofanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam jana. Timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara kwa wateja binafsi Benki ya NBC, Elibariki Masuke (Kulia) akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake wakubwa kabla ya kuelekea Uwanja wa Taifa wa Benjamin Mkapa kushudia mechi hiyo.

Meneja Mahusiano wa Benki ya NBC , Brendansia Kileo (katikati) akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake wakubwa kabla ya kuelekea Uwanja wa Taifa wa Benjamin Mkapa kushudia mechi hiyo.

“Tumetumia mechi hii kubwa kuwakaribisha wateja wetu wa tawi letu jipya lililopo wilayani Kigamboni lengo likiwa ni kufurahi nao katika ligi hii. Zaidi ya wateja 70 wilayani humo walipata fursa ya kutazama mechi hiyo kwa udhamini wa benki ya NBC ambapo tuliweza kuwapatia usafiri wa kwenda uwanjani na kurudi majumbani mwao wakiwa salama kabisa,’’ – David Kigwile, Kaimu Mkuu wa Idara ya Masoko,  Benki ya NBC.



Mbali na kutoa fursa kwa wapenzi wa soka kufuatilia mechi hiyo kupitia screen kubwa pia walipata fursa ya kupata huduma mbalimbali za kifedha kutoka benki ya NBC kupitia maofisa wa benki hiyo waliokuwa wakitoa huduma mbalimbali ikiwemo kufungua akaunti mbalimbali pamoja na kufanya mihamala ya kifedha wakiwa maeneo hayo pamoja na viunga vya uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.


 

No comments: