SERIKALI INATAMBUA MCHANGO WA WAGANGA WA TIBA ASILI, BADO HAIJATHIBITISHA DAWA YA ASILI KUTIBU KIFUA KIKUU

Meneja matokeo ya kimkakati katika Mradi wa USAID, Modestus Kamoga akizungumza katika mdahalo uliofanyika jijini Dar es Salaam leo Oktoba 28, 2022. 
Mratibu wa Ugonjwa wa Kifua Kikuu, kutoka Ofisi ya Mkoa wa Tabora,  Idara ya Afya, Benedicto Komba akizungumza katika mdahalo uliofanyika jijini Dar es Salaam leo Oktoba 28, 2022. 
Mratibu wa Ugonjwa wa Kifua Kikuu Wilaya ya igunga, Dkt. Justina Mkome akizungumza katika mdahalo uliofanyika jijini Dar es Salaam leo Oktoba 28, 2022. 



Baadhi ya Washiriki wakiwa kwenye mdahalo ulioratibiwa na Policy Forum jijini Dar es Salaam leo Oktoba 28, 2022.
Mmoja ya washiriki wakichangia mada katika Mdahalo uliofanywa na Policy Forum leo  Oktoba 28, 2022 jijini Dar  es Salaam.

SERIKALI inatambua na kuthamini mchango wa waganga wa tiba asili ndio maana inaelekeza kutumia dawa ambazo zimefanyiwa utafiti na kuthibitishwa kwamba zinaweza kumuua Bakteria wa Kifua Kikuu.

"Kwahiyo Mchango wa Tiba asili katika kutibu Kifua kikuu serikali bado haijathibitisha mpaka sasa, tunatumia dawa zilizoainishwa na zilizothibitishwa na serikali kutibu Ugonjwa huo."

Hayo yamesemwa na Mratibu wa Ugonjwa wa Kifua Kikuu Wilaya ya Igunga, Dkt. Justina Mkome wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Oktoba 28, 2022. Wakati wa mdahalo unaoendeshwa na Policy Forum. Amesema kuwa katika juhudi za serikali za kupambana na ugonjwa wa Kifua Kikuu ni pamoja na kuwatembelea Waganga wa tiba asili ili kufanya vipimo vya Ugonjwa huo na kuwatibu mapema.

Amesema kuwa Katika Wilaya ya Igunga waliona wagonjwa wengi au Wateja wengi wanapotea na wengine wanafariki dunia wakaona wafanye utafiti mfupi wakaona wateja wengi wanachelewa kufika kwenye vituo vya kutolea huduma kwa sababu wanaenda Kupata tiba kwa waganga wa tiba za asili.

"Kwahiyo tuliamua kufika kwa baadhi ya wanganga wa tiba asili ambao tuliweza kukutana na waganga wa 24 na tuliweza kufanya uchunguzi kwa Wananchi 500 na tuliweza kuwapata wateja wapya wa Kifua kikuu 40.

Kwa hiyo ni kitu kikubwa sana katika Wilaya ya Igunga kwa sababu tuliona kesi ambazo tulizipata kwa waganga wa tiba asili tulikuwa tumezimisi na tuliweza kuzipata kwa waganga wa tiba asili." Amesema Dkt. Mkome.

 Kwa Upande wake Mratibu wa Ugonjwa wa Kifua Kikuu, kutoka Ofisi ya Mkoa wa Tabora,  Idara ya Afya, Benedicto Komba amesema wananchi hapa nchini bado wanaimani sana na tiba asili hivyo serikali imeona umhimu wa kushirikiana na Waganga wa Tiba asili ili kuweza kuwaibuwa wangonjwa wa Kifua kikuu.

"Tuliona tuwashirikishe hawa Waganga wa Tiba asili. kwa hiyo bila kuwatumia waganga hao hatuwezi kufanikiwa kuwapata wangonjwa wengi kama tuliowakuta katika wakipata kwa waganga wa tiba asili ambapo wanajamii wetu wanakwenda kwao kupata matibabu ya maradhi mbalimbali" Amesema Dkt. Komba

Amesema kuwa akithibitika na Ugonjwa wa Kifua Kikuu kwa Mganga wa Tiba asili wanashirikiana na ili kuweza kumpa tiba ambazo zimethibitishwa na Serikali.

Kwa Upande wa Washiriki wakichangia Mada Katika Mdahalo huo wamesema kuwa elimu zaidi itolewe kukabilia na Ugonjwa wa Kifua Kikuu Nchini.

Amesema kuwa jamii haijui tofauti ya Kifua kikuu na Ukimwi hivyo Elimu itolewe katika Jamii pamoja na Waliopo kwenye taasisi ya elimubwapewe elimu kuhusu Ugonjwa wa Kifua Kikuu.

No comments: