ASILIMIA 90 YA MADEREVA NA MAKONDAKTA HAWANA MIKATABA YA KAZI- MZUMBE
Mhadiri wa Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Godbertha Kinyondo akitoa ufafanuzi kwa madereva na makondakta wa jijini Dar es Salaam leo Oktoba 28, 2022. wakati wa kuwasilisha matokeo ya utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu Mzumbe.
UTAFITI uliofanywa na Chuo Kikuu Mzumbe umeonesha kuwa zaidi ya Asilimia 90 ya Madereva na Makondakta wa Daladala wa jijini Dar es Salaam hawana mikataba inayotambua kazi zao, Mikataba iliyopo ni ya Chombo na si ya Mfanyakazi.
Mtafiti kutoka Chuo Kikuu Mzumbe, Aloyce Gervas, akizungumza wakati wa Kuwasilisha Utafiti uliofanywa na chuo Kikuu Mzumbe kuanzia Mwaka 2007 katika Sekta ya Usafirishaji na manufaa ua Vikundi vya daladala na Bodaboda amesema kuwa Wafanyakazi wa Daladala hawana mikataba ya kazi ambayo inaonesha haki na stahili zao.
Ametoa wito kwa Mamlaka zote zinazofatilia maslahi ya waajiriwa waweze kuangalia sekta hiyo muhimu ya wasafirishaji ambayo ni moja ya sekta mhimu na inayochangia katika uchumi wa nchi.
Katika matokeo hayo imeonesha kuwa asilimia 99 ya wanaume waliohojiwa kuwa asilimia 17 wamejiunga na hifadhi za jamii, asilimia 16 tu ndio wamejiunga na bima ya afya na asilimia 84 hawana bima za afya huku asilimia 89 hawalipi bima ya afya kwasababu wanaona sio mhimu. Pia wanaona kama ni Urasimu tu.
Kwa Upande wa Mhadiri wa Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Godbertha Kinyondo amesisitiza madereva na Makondakta wa Daladala na Bodaboda wajiunge na vyama vya wafanyakazi ili waweze kupata vitu vya msingi ambavyo vipo katika chama au kikundi.
Pia amewaasa wajiunge na bima ya afya na Mifuko ya Pensheni ili waweze kujikimu uzeeni na pale ambapo wanapata maradhi mbalimbali.
Kwa upande wa Vijana amewaasa kujiunga na mifuko hiyo ili ije kuwasaidia pale wanapofikisha miaka zaidi ya 50.
"Vijana Makondakta na Madereva wameitikia kujiunga na mifuko hiyo kwa furaha kuwa wataenda kujiunga." Amesema Dkt. Kinyondo
Kwa Upande wa Amani Mwinyimvua kutoka TAROT amewapa maelekezo wadereva na makondakta pamoja na wale waliopo katika sekta ya Usafirishaji amewaelekeza namna ambavyo wanaweza kujiunga na vikundi hatimaye kujiunga na Vyama vya wafanyakazi.
Kwa Upande wa Katibu wa Umoja wa Madereva na Makondakta wa magari yaendayo Uzaramuni (UMAM GROUP), Maulid Selemani amewashukuru TAROTU ambao wamewasaidia kujiunga na vikundi mbalimbali hadi wameweza kujimilikisha magari manne.
Mpaka sasa naamini kwa hatua tuliyotokea nyuma na sasa naona kunamabadiliko makubwa naamina tunaweza kufanya makubwa zaidi kwa kupitia Mzumbe laiti kama tungewapata Mzumbe tangu kipindi cha nyuma nadhani saivi tungekuwa mara mbili yake." Amesema Selemani
Hivyo Mifuko ya bima ya afya na Mifuko ya Pensheni nchini wanaahimizwa kutoa elimu ya huduma wanazozitoa ili jamii ijue umhimu wa suala hilo.
Baadhi ya Madareva na Makondakta wameeleza kuwa Mikataba wanayoipata ni ile ambayo wanaipata wakati wanenda kusajili chombo ili kiingie barabarani na waajiri wanatumia mikataba hiyo kuwapa mishahara kwa mwezi mmoja au miwili.
Amesema kuwa baada ya miezi miwili au mitatu kupewa mishahara hawapati tena stahili zao baada ya hapo hawapati.
Pia wamepewa viakisi mwanga ambavyo vinaujumbe mbalimbali ambazo zitawawezesha kujipatia fursa mbalimbali ambazo zinatolewa hasa za mikopo na fursa nyingine za elimu.
Mtafiti kutoka Chuo Kikuu Mzumbe, Aloyce Gervas, akizungumza na madereva na Makondakta wa sekta ya Usafirishaji jijini Dar es Salaam leo Oktoba 28, 2022 wakati wa kutoa matokeo ya Utafiti uliofanywa kuanzia 2007 hadi sasa yanatolewa matokeo.
Katibu wa Umoja wa Madereva na Makondakta wa magari yaendayo Uzaramuni (UMAM GROUP), Maulid Selemani akiwapa ushuhuda Madereva na Makondakta wa jijini Dar es Salaam jinsi walivyojiunga na kuendeleza Chama cha na kufanikiwa kuwa na uongozi bora ikiwa pamoja na kununua Magari manne kwaajili ya kupunguza makali ya Ajira katika chama chao.
Mhadiri wa Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Godbertha Kinyondo akitoa ufafanuzi kwa madereva na makondakta wa jijini Dar es Salaam leo Oktoba 28, 2022. wakati wa kuwasilisha matokeo ya utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu Mzumbe.
Amani Mwinyimvua kutoka TAROT akifafanua jinsi ya kutengeneza Umoja au chama kwa Mdereva na Makondakta jijini Dar es Salaam leo Oktoba 28, 2022.
Madereva na Makondakta Wazee wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kupewa matokeo ya utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu Mzumbe.
Picha ya Pamoja
Baadhi ya Madereva na Makondakta wakiuliza masuali na kuchangia mada wakati wafanyakazi chuo Kikuu Mzumbe wakitawanya Utafiti walioufanya juu ya Masuala ya Bima ya Afya na Mfuko ya Pensheni katika Sekta ya Usafirishaji jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Madereva na Makondakta wakisikiliza wakati wafanyakazi chuo Kikuu Mzumbe wakitawanya Utafiti walioufanya juu ya Masuala ya Bima ya Afya na Mfuko ya Pensheni katika Sekta ya Usafirishaji jijini Dar es Salaam.
No comments: