TUWEKE SAWA SHERIA, SERA TUTADHIBITI TAKA NGUMU - NIPE FAGIO

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
TAASISI ya Nipe Fagio imeshauri Serikali kuweka sawa Sheria na Sera ili kudhibiti Takataka ngumu katika mazingira yanayoizunguka Jamii.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam katika Siku ya Usafi Duniani, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Ana Rocha amesema takataka aina ya Plastiki zinaongoza kwa uchafuzi wa mazingira kwa kiasi kikubwa duniani kote.

Rocha ameshauri kwa Mamlaka husika kuweka Sheria sawa ili kuzuia Plastiki ambazo zinasababisha uchafuzi mkubwa wa mazingira, amesema kwa kuweka Sheria, Sera sawa kutakuwa na mabadiliko makubwa katika usafi wa mazingira.

“Tumekuja hapa Baharini kufanya usafi, kutokana na Taka nyingi zinakuja Baharini kutoka kwenye Mito baada ya kutoka kwenye matumizi mbalimbali. Hapa tumekuja kutoa elimu kwa jamii kuhusu namna ya kudhibiti Taka maana kufanya usafi wa mazingira ni kazi ngumu”, amesema Rocha.

Rocha amesema wamefanya zoezi hilo la usafi ili kukusanya takwimu kama Taasisi ili kusaidia katika udhibiti wa Takataka hizo amesema taarifa hizo za Takataka zinahitajika Kitaifa na Ulimwenguni kote ili kuthibiti uchafu katika mazingira.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Environmental Conservation Community of Tanzania (ECCT), Lacky Michael amesema jamii inaendelea kuitika na kupokea elimu ya utunzaji wa mazingira na udhibiti wa Takataka.

“Wananchi waendelee kudhibiti Taka majumbani mwao, tunategemea nchi itakuwa katika hali ya usafi kupitia Kampeni mbalimbali za kuhamasisha usafi”, amesema.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi wa Nipe Fagio, Ana Rocha akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam katika zoezi la usafi ikiwa ni katika Siku ya Usafi Duniani

Usafi ukiendelea.
Takataka zilizopo kwenye baadhi ya fukwe za jijini Dar es Salaam.

No comments: