Mganga Mkuu Hospitali ya Rufaa Temeke Aongoza Maadhimisho ya Siku ya Usafi Duniani, Temeke.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Temeke Dkt. Joseph Kimaro, ameongoza kufanya usafi katika maadhimisho ya usafi Duniani yanayofanyika Septemba 17 kila mwaka ambapo kwa Temeke yamefanyika Keko Mwanga A na B kwa ushirikiano wa Taasisi zisizo za kiserikali zikiwemo, HUDEFO, TCCI, Mazingira Plus, ETE Worldwide Solutions, Maafisa Mazingira kutoka manispaa ya Temeke,Maafisa Afya kutoka hospital ya Temeke na ofisi ya kata,Viongozi wa dini,wenye Viti wa Serikali ya Mtaa ya keko Mwanga A na B.
Usafi huo umefanyika katika eneo la Makaburi ya Keko mwanga ambapo awali palikuwa pamegeuzwa kama eneo la kutupia takataka kutoka majumbani na maeneo jirani.
Akizungumza na wakazi wa Keko Mwanga Dkt. Joseph Kimaro alitoa rai kwa wakazi wa eneo ilo kuacha kutupa taka katika makaburi hayo ili eneo hilo liendelee kuwa safi na kupunguza vifo vya watoto chini ya Miaka mitatu kwa kuwa wengi huathirika kwa kuhara kutokana na kula kila kitu ikiwemo na vitu vichafu, na kuhimiza kuwa zoezi hilo liwe endelevu.
Dkt. Kimaro amefurahishwa na ushiriki wa wadau mbalimbali katika zoezi la usafi lilofanyika eneo la Makaburi ya keko Mwanga A na pia amekaribisha wananchi katika hospitali ya Temeke na kumshukuru Rais Samia Suluhu kwa Mapinduzi makubwa kwenye sekta ya Afya,hospital ya Temeke imeongezewa vifaa Tiba na mashine mbalimbali hivyo huduma vimezidi kuimarika.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Temeke, Dkt. Joseph Kimaro (wa pili kushoto) pamoja na wadau wengine wa Mazingira wakifanya usafi katika eneo la Keko Mwanga A, Temeke
Baadhi ya wadau mbalimbali wa mazingira pamoja na wakazi wa Keko Mwanga A na B wakiwa wanafanya usafi katika maadhimisho ya siku ya Usafi Duniani
Muonekano wa Makaburi ya Keko Mwanga kabla na Baada ya kufanyiwa usafi
Wadau wa Mazingira pamoja na wakazi wa Keko Mwanga A na B wakipata elimu ya Mazingira baada ya kumaliza kufanya usafi
Picha ya pamoja.(Picha zote na Fredy Njeje- Mdau wa Mazingira, ETE Worldwide Solutions)
No comments: