Benki ya NBC Yakabidhi Msaada wa Matenki ya Maji Sekondari Mbeya
Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imekabidhi msaada wa Matenki ya maji manne yenye jumla ya ujazo wa lita 40,000 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 10 kwa uongozi wa Shule ya Sekondari ya Mbeya ikiwa ni mwendelezo wa mkakati wa benki hiyo kuunga mkono jitihada za serikali za kuboresha sekta ya elimu hapa nchini.
Msaada huo ulikabidhiwa kwa uongozi wa shule hiyo na Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Mbeya Bi Asia Mselemu wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo iliyohudhuliwa na walimu, wanafunzi, baadhi ya wadau wa elimu mkoani humo, wafanyakazi wa benki ya NBC na viongozi waandamizi wa serikali wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Dkt Rashid Chuachua.
Akizungumza mara tu baada ya kupokea msaada huo sambamba na uongozi wa shule hiyo Dkt Chuachua pamoja na kuishukuru benki ya NBC kwa jitihada hizo, alisema msaada huo unakwenda sambamba na jitihada za serikali za kuboresha hali ya elimu mkoani humo na kwamba msaada huo utasaidia kupunguza changamoto ya muda mrefu ya upatikanaji wa maji safi kwa walimu na wanafunzi shuleni hapo.
“Kama inavyofahamika kwasasa serikali kupitia jitihada za Mheshimiwa Rais Samia Suluhu ipo kwenye mpango mkubwa wa kuboresha upatikanaji wa elimu bora hapa nchini, mkakati ambao unahusisha mambo mengi ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa, kuongeza idadi ya walimu na maslahi yao na mambo mengine mengi.’’
“Hivyo, tunafarijika zaidi kuona kwamba wadau kama benki ya NBC wanajitokeza kuunga mkono jitihada hizi kwa namna mbalimbali ikiwemo hii ya upatikanaji wa maji safi kwa walimu na wanafunzi kwenye shule zetu…tunashukuru sana NBC,’’ alisema.
Akizungungumzia msaada huo, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Bw Francis Mwakihaba pamoja na kuishukuru benki ya NBC kwa msaada huo alisema kupitia msaada huo wanafunzi wa shule hiyo takribani 1464 na watumishi 71 wakiwemo walimu wamehakikishiwa upatikanaji wa huduma ya maji safi kwa uhakika hali ambayo itaokoa nguvu na muda mwingi uliokuwa ukitumiwa na wanafunzi kutafuta huduma hiyo muhimu na kuathiri muda wao wa masomo na usalama wao.
“Ni msaada ambao utakuwa na faida nyingi sana hususani kitaaluma kwasababu wanafunzi watakuwa na muda wa kutosha kujisomea badala ya kuhangaika kutafuta maji. Hata hivyo ni ombi letu tena kwa NBC au wadau wengine waone namna ya kutuchimbia visima ili viwe vyanzo vya maji yatakayokuwa yanahifadhiwa kwenye matenki haya kwa uhakika zaidi,’’ aliomba.
Kwa upande wake Bi Asia Mselemu alisema kuwa benki hiyo imejitolea kusaidia katika kuboresha ustawi wa jamii kupitia misaada ya kijamii ikiwemo elimu na kwamba wameguswa sana na suala la changamoto ya upatikanaji wa maji safi shuleni hapo, sababu iliyosababisha wao kuchukua hatua hiyo ili kuwasaidia wanafunzi na walimu kuepukana na changamoto hiyo.
“Ni furaha kwetu kuwa sehemu ya kutatua changamoto kwenye sekta muhimu kama hii. Huu ni mwendelezo tu wa jitihada zetu kwenye maeneo mengi ya kijamii kupitia mpango wetu wa uwajibikaji kwa jamii. Tunawashukuru sana walimu na wafaunzi wa shule ya sekondari Mbeya kwa kutona NBC kama mdau muhimu kwenye kutatua changamoto hii.’’
“Nasi tunaahidi kuendelea kushirikiana nao kwenye mambo mengine pia. Wito wangu kwa wana jamii wa shule hii ni wao kuyatunza vema matenki haya ili yatumike kwa muda mrefu kama ilivyokusudiwa.’’ Alisisitiza.
Akitoa shukrani zake kwa niaba ya wanafunzi wenzake wa shule hiyo, mwanafunzi Dorcas Jerry alisema msaada huo umewanusuru dhidi ya changamoto iliyokuwa ikiwalazimu kutumia sehemu ya muda wa masomo binafsi kwenda kutafuta maji badala ya kujadili kuhusu masomo yao.
“Msaada huu pia una faida kiafya hususani kipindi cha hedhi kwa sisi wanafunzi wa kike kwa kuwa huwa tunahitaji usafi wa hali wa juu hivyo tunahitaji maji ya kutosha. Tunawashukuru sana benki ya NBC kwa msaada huu na tunaahidi kufanya vizuri zaidi kimasomo,’’ alisema.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Dkt Rashid Chuachua (wa pili kulia) akipeana mkono na Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Mbeya Bi Asia Mselemu ikiwa ni ishara ya kupokea na kushukuru msaada wa Matenki ya maji manne yenye jumla ya ujazo wa lita 40,000 yenye na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 10 yaliyotolewa na benki hiyo kwa ajili ya Shule ya Sekondari ya Mbeya ili kuunga mkono jitihada za serikali za kuboresha sekta ya elimu hapa nchini. Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mstahiki Meya wa jiji la Mbeya Dour Mohammed Issa (Kushoto).
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Dkt Rashid Chuachua akizungumza na baadhi ya wadau wa elimu mkoani humo pamoja na wanafunzi wakati wa hafla fupi ya kupokea msaada wa Matenki ya maji manne yenye jumla ya ujazo wa lita 40,000 yaliyotolewa na benki ya NBC kwa ajili ya Shule ya Sekondari ya Mbeya ili kuunga mkono jitihada za serikali za kuboresha sekta ya elimu hapa nchini. Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo. Wanaomsikiliza ni pamoja na Mstahiki Meya wa jiji la Mbeya Dour Mohammed Issa (wa pili kushoto) Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Mbeya Bi Asia Mselemu na Mkuu wa shule hiyo Bw Francis Mwakihaba.
Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Mbeya Bi Asia Mselemu (kushoto) akikaribishwa na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mbeya wakati wa hafla fupi ya kukabidhi msaada wa Matenki ya maji manne yenye jumla ya ujazo wa lita 40,000 yaliyotolewa na benki hiyo kwa ajili ya shule hiyo ili kuunga mkono jitihada za serikali za kuboresha sekta ya elimu hapa nchini. Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo. Wengine ni walimu, wafanyakazi wa benki ya NBC na viongozi waandamizi wa serikali.
Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Mbeya Bi Asia Mselemu (kulia) akipokea chetu maalum cha kutambua jitihada za benki hiyo katika kusaidia jamii kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Dkt Rashid Chuachua wakati wa hafla fupi ya kukabidhi msaada wa Matenki ya maji manne yenye jumla ya ujazo wa lita 40,000 yaliyotolewa na benki hiyo kwa ajili ya Shule ya Sekondari ya Mbeya ili kuunga mkono jitihada za serikali za kuboresha sekta ya elimu hapa nchini. Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo.
Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Mbeya Bi Asia Mselemu akizungumza na baadhi ya wadau wa elimu mkoani humo pamoja na wanafunzi wakati wa hafla fupi ya kukabidhi msaada wa Matenki ya maji manne yenye jumla ya ujazo wa lita 40,000 yaliyotolewa na benki hiyo kwa ajili ya Shule ya Sekondari ya Mbeya ili kuunga mkono jitihada za serikali za kuboresha sekta ya elimu hapa nchini. Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo.
Mstahiki Meya wa jiji la Mbeya Dour Mohammed Issa akizungumza na baadhi ya wadau wa elimu mkoani humo pamoja na wanafunzi wakati wa hafla fupi ya kupokea msaada wa Matenki ya maji manne yenye jumla ya ujazo wa lita 40,000 yaliyotolewa na benki ya NBC kwa ajili ya Shule ya Sekondari ya Mbeya ili kuunga mkono jitihada za serikali za kuboresha sekta ya elimu hapa nchini. Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo.
Akitoa shukrani zake kwa niaba ya wanafunzi wenzake wa shule hiyo, mwanafunzi Dorcas Jerry (pichani) alisema msaada huo umewanusuru dhidi ya changamoto iliyokuwa ikiwalazimu kutumia sehemu ya muda wa masomo binafsi kwenda kutafuta maji badala ya kujadili kuhusu masomo yao.
No comments: