WAFANYABIASHARA WA VINYWAJI PAMOJA NA WATUMIAJI WATAKIWA KUWA NA UTARATIBU WA KUHAKIKI UBORA KABLA YA KUVITUMIA


Wafanyabiashara wa Vinywaji pamoja na watumiaji wametakiwa kuwa na utaratibu wa kuhakiki ubora wa vinywaji kabla ya kuvitumia kwa kutumia app maalumu ya Hakiki stempu ili kutambua bidhaa feki ambazo zinaweza kuhatarisha afya zao.

Wito huo umetolewa hivi karibuni na Balozi Mradi wa Stempu za Kodi za Kielektroniki (ETS) kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Ruekaza Rwegoshora wakati akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea maonesho ya Nanenane yaliyofanyika kitaifa mkoani Mbeya wiki iliyopita.

Alisema TRA inapenda kuwahamasisha wafanyabiashara na wananchi wanaotumia bidhaa kama mvinyo wa zabibu, matunda aina mbalimbali, pombe kali, bia, sigara na aina zingine za vileo kushiriki kulinda afya zao kwa kuzihakiki kabla ya kuzitumia.

Rwegoshora alisema App ya Hakiki stempu inauwezo wa kutambua uhalali wa bidhaa za vinywaji ambazo zipo sokoni ambapo mtumiaji atapaswa kuwanayo katika simu janja na kufanya uhakiki wa bidhaa iwapo inafaa kwa matumizi ya binadamu.

"Hii app maalumu ni bure na inapatikana katika hizi simu janja kazi yake ni kuhakiki ubora wa vinywaji vyako, lengo la kuhakiki ubora wa bidhaa za vinywaji ni kwa sababu kuna aina nyingi za bidhaa hizo siyo rahisi kufahamu ubora wake," alisema

Amesisitiza kuwa kwa kutumia mfumo huo wa app mfanyabiashara na mtumiaji ataweza kupata taarifa sahihi kuhusu ilipotoka bidhaa,ilipotengenezwa,na lini itaisha muda wake wa matumizi hivyo kumfanya mlaji wa bidhaa husika kuwa salama.

Kwa Upande wake balozi mwingine wa ETS kutoka TRA, Lewis Rwenyagira alisema ETS ni alama maalum zinazobandikwa au kuchapishwa katika bidhaa ili kuonyesha kuwa ni halalìna imezalishwa au kuingizwa nchini na mfanyabiashara anayetambulika na amelipa kodi ya ushuru wa bidhaa stahiki.

Hata hivyo alisisitiza kuwa App hiyo ya kuhakiki bidhaa inafaida nyingi kwa wafanyabiashara hasa pale wanapokwenda kununua vinywaji kwani itawasaidia kutambua bidhaa feki pamoja na kufahamu ubora wake hivyo ili kumlinda mteja.


Ma afisa mradi wa ETS kutoka TRA, Bw. Ruekaza Rwegoshora (L) Bw. Lewis Rwenyagira,(C ) na balozi wa ETS/Hakiki stempu wakitoa ufafanuzi kwa wanahabari (hawapo pichani) jinsi mfumo wa kielektroniki wa kuhakiki stempu unavyofanya kazi katika viwanja vya maonesho ya kilimo Nanenane yaliyofanyika kitaifa jijini Mbeya mwaka huu.






Ma afisa mradi wa ETS kutoka TRA, Bw. Ruekaza Rwegoshora (L) Bw. Lewis Rwenyagira,(C ) na balozi wa ETS/Hakiki stempu wakitoa ufafanuzi kwa wanahabari (hawapo pichani) jinsi mfumo wa kielektroniki wa kuhakiki stempu unavyofanya kazi katika viwanja vya maonesho ya kilimo Nanenane yaliyofanyika kitaifa jijini Mbeya mwaka huu.







Balozi wa ETS kutoka TRA akimsaidia mfanyabiashara kupakua app ya Hakiki stempu kwa ajili ya kuhakiki ubora wa bidhaa, katika viwanja vya maonesho ya kitaifa ya kilimo Nanenane jijini Mbeya.



Maofisa wa Tra na mabalozi wa ETS wakitoa elimu wa wafanyabiashara wa vinywaji waliotembelea viwanja vya nanenane jinsi ya kupakua na kutumia app ya hakiki stempu kwa njia ya kielektroniki (ETS). Sikukuu za kitaifa za maonesho ya nanenane zimefanyika jijini Mbeya wiki iliyopita kwa mwaka huu wa 2022 na kuhudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan.

No comments: