Vodacom yakabidhi zawadi za awamu ya sita promosheni ya M-Pesa Imeitika jijini Dar es salaam

Kampuni ya teknolojia na mawasiliano ya Vodacom Tanzania Plc, imekabidhi zawadi kadhaa kwa washindi wa awamu ya sita ya M-Pesa Imeitika. Akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano hayo, Mkuu wa Mauzo Vodacom kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Brigita Shirima, amesema nina furaha kubwa sana kuwa nanyi leo hapa Viwanja vya Barafu, Mburahati, tunapokabidhi zawadi kwa washindi wetu wa awamu ya sita wa kampeni ya “M-Pesa Imeitika”.

Kampeni hii ni muendelezo wa juhudi zetu za kuipeleka Tanzania katika Ulimwengu wa kidijitali hususan katika sekta ya kifedha. Kampeni hii ni muendelezo wa juhudi za vodacom za kuipeleka Tanzania katika Ulimwengu wa kidijitali hususani katika sekta ya kifedha.

Shirima amefafanua kuwa kampeni hiyo inahusisha zawadi kama pikipiki, bajaji, mafuta kwa wamiliki wa magari pamoja na zawadi kubwa ya nyumba; na kwamba inaendana kabisa na malengo ya serikali ya kuhakikisha Tanzania inaingia katika ulimwengu wa kidijitali Aliendelea kusema, “Hii imekuja ikiwa ni juhudi zetu za kuwarudishia tabasamu wateja wetu wapendwa, haswa baada ya serikali kupunguza tozo za miamala ya simu, sisi kama kampuni inayopigania kuipeleka Tanzania katika ulimwengu wa kidijitali tumeona ni vema tukawapa Watanzania kitu kidogo cha kujivunia kwa vile pia hii inaendana kabisa na malengo ya serikali ya kuhakikisha kwamba Tanzania inaingia katika ulimwengu wa kidijitali”.

Katika kutoa huduma anuwai, moja ya faida ambayo tumeiona kwa watumiaji, ni kupungua kwa uhitaji wa kutumia pesa taslimu katika miamala yao ya kila siku. Si lazima tena mtu kuwa na pesa mkononi kwa kila jambo. Hii haiongezi tu kasi ya kukamilisha miamala, bali pia huongeza usalama binafsi kwa mtumiaji na kutoa fursa ya usimamizi bora wa fedha za mteja. Vodacom imedhamiria kuboresha hali ya maisha na uchumi wa Watanzania wote.

Kupitia kampeni hii, tunalenga kuongoza njia kwenye ulimwengu wa huduma za kifedha kidijitali na kufiia mfumo wa M-Pesa kuwa ni sehemu ya maisha ya kila siku kwa wateja wetu. Kwa sasa huna sababu ya kubeba pesa taslimu, kwa vile kila utakacholipia au kutuma pesa kutoka M-Pesa basi unajiongezea nafasi ya kushinda, lakini pia unajiepusha na hatari zinazoambatana na kubeba pesa taslimu.

Niwapongeze washindi hawa wote wa leo kutoka katika ukanda wetu, nikiamini kabisa kwamba zawadi hizi sio tu zitawasaidia kwenye usafiri lakini pia itakuwa ni chanzo cha kuwaingizia fedha na pia ni ajira kwa watu walio karibu nao. Alimaliza kusema Shirima.



Mkuu wa Mauzo wa kanda ya Dar es salaam na Pwani Vodacom Tanzania PLC, Brigita Shirima (kulia) akimkabidhi funguo mshindi wa Bajaj wa promosheni ya M-Pesa Imeitika kutoka Kimara jijini Dar es Salaam, Magdalena Magoma Moke wakati wa hafla ya kukabidhi Bajaj moja na Bodaboda tano kwa washindi wa awamu ya sita iliyofanyika viwanja vya Barafu Mburahati jijini humo.

Mkuu wa Mauzo wa kanda ya Dar es salaam na Pwani Vodacom Tanzania PLC, Brigita Shirima (wapili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa Bodaboda wa promosheni ya awamu ya sita ya M-Pesa Imeitika jijini Dar es salaam









No comments: