RC KUNENGE ATOA HAMASA KWA WAKAZI KANDA YA MASHARIKI KUTEMBELEA MAONESHO MOROGORO
Na Khadija Kalili Kibaha
MKUU wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge pichaniamewataka wakazi wa Mikoa inayounda Kanda ya Mashariki kujitokeza kwa wingi kwenye maonesho ya sherehe za wakulima yanayofahamika kama nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya Julius Kambarage Nyerere Mkoani Morogoro.
Akizungumza leo Julai 30, 2022 katika mkutano na Waandishi wa Habari ambapo amezungumza kwa niaba ya Wakuu wa Mikoa inayounda Kanda ya Mashariki amesema kuwa maonesho hayo yatazinduliwa kesho Julai 31 na yatafika kileleni ifikapo Agosti 8 mwaka huu.
RC Kunenge ameitaja mikoa ambayo inaunda Kanda ya Mashariki kuwa ni Morogoro,Tanga, Dar es Salaam na Pwani pia alitoa wito kwa wakazi wa Mikoa hiyo kujitokeza kwa wingi na kujumuika katika maonesho hayo kwani wataweza kujifunza na kupata elimu juu ya mambo mbalimbali ikiwemo teknolojia ya kilimo, ufugaji na uvuvi.
Amesema kuwa maonesho hayo yatazinduliwa ifikapo Agosti 2 mwaka huu.
Amesema kuwa kauli mbiu ya mwaka huu ni "Kilimo ni biashara shiriki kuhesabiwa kwa mpango bora wa kilimo, mifugo na uvuvi."
Amesema kuwa burudani mbalimbali zitakuwepo kwenye maonesho hayo.
No comments: