SERIKALI YATOA FURSA KWA WAKULIMA WA ZAO LA TUMBAKU NA PAMBA


Wakulima wa mazao ya Tumbaku na Pamba mkoani Shinyanga wamepewa jukumu la kulima zaidi mazao hayo katika maeneo yao baada ya kuhakikishiwa Soko la uhakika na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akizungumza katika ziara Wilayani Kahama mkoani humo, Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo amesema kuwa ameagizwa na Rais Samia Suluhu kuwapa ujumbe Wakulima wa mazao hayo kulima zaidi kwa kuwa kuna Soko la uhakika la mazao hayo.

“Nimezungumza na Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe kuhusu mpango wa Wakulima, ameniambia kuwa mpango ni kuzalisha Tani Laki moja au Kilogramu Milioni 100 za mazao haya, maana yake ninyi Wakulima muende kulima maeneo makubwa na Kilimo kikubwa ili uzalishaji uanze kupanda kuanzia sasa”, amesema Chongolo.

Chongolo amesema Mnunuzi mkubwa wa zao hilo la Tumbaku mkoani Morogoro, alikuwa na changamoto lakini hadi sasa changamoto hizo tayari zimetatuliwa na hivi karibuni Kiwanda hicho kitawashwa kwa ajili ya kufanya uzalishaji, amesema Kiwanda hicho kinahitaji Kilogramu zaidi ya Milioni 30 na zaidi hivyo Wakulima hao wanapaswa kuchangamkia fursa kulima zaidi.

“Tumbaku inauzwa kwa Dola 1.65 ipo hapa inauzwa kwa madaraja ukiitunza vizuri zaidi inaenda hadi daraja la juu inauzwa Shilingi 5000 kwa kilo, sawa na Dola mbili na zaidi, zao la Pamba nalo limeni kwa kiwango kikubwa kwa sababu Soko lipo”, ameeleza

Chongolo amesema zao hilo litauzwa kwa Shilingi 1560 kwa Kilo tofauti na mwaka jana ambapo Kilo ilikuwa Shilingi 1050 na ‘Organic’ inauzwa hadi Shilingi 1700 kwenye Soko hadi sasa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Tumbaku Tanzania, Stanley Mnozya ameishukuru Serikali ya Tanzania kuweka mazingira wezeshi kwa Wakulima hao wa zao la Pamba nchi nzima kwa kuondoa changamoto zilizokuwa zinawakabili Wakulima hao.

“Miaka mitano hadi Sita iliyopita, Sekta ya Tumbaku iliyumba sana baada ya kuondoka Mnunuzi wa zao hili, tunashukuru baada ya Mnunuzi kurudi anataka kiasi cha tani Milioni 30 maeneo yote”.

“Mwakani  tunategemea kuwa na Kilogramu 100 Milioni tofauti na zamani tulikuwa na Kilogramu 70 Milioni, na sasa Kiwanda kilichokuwa kimesimama kwa miaka mitatu au minne kule Morogoro kinaenda kuwashwa ,kwa hiyo ni fursa kubwa kwa Wakulima”, amesema Mnozya.





Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo (wa tatu kulia ) akisomewa taarifa fupi na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Tumbaku Tanzania, Stanley Mnozya baada ya kuona uzalishaji mkubwa wa zao la Tumbaku alipotembelea Ghala la kuhifadhia tumbaku la Chama Kikuu cha Ushirika cha Kahama (KACU) na baadae kuzungumza na Viongozi pamoja na wafanyakazi





Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo (wa tatu kulia ) akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Tumbaku Tanzania, Stanley Mnozya baada ya kuona uzalishaji mkubwa wa zao la Tumbaku alipotembelea Ghala la kuhifadhia tumbaku la Chama Kikuu cha Ushirika cha Kahama (KACU) na baadae kuzungumza na Viongozi pamoja na wafanyakazi

Tumbaku ikiwa imehifadhiwa kwenye ghala tayari kwa biashara





Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo (katikati)akizungumza na wafanyakazi na viongozi wa katika ghala la Chama Kikuu cha Ushirika cha Kahama (KACU).
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo (kulia)akimuangalia Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ndugu Ngemela Lubinga akijaribu kufanya mazoezi na kifaa maalumu cha kisasa katika kitengo cha tiba za mazoezi fiziotherapia katika jingo la wagonjwa wa nje (OPD) katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akihutubia wakati wa shina namba 1, Tawi la Mayila Kata ya Nyehongwe, Kahama mkoani Shinyanga linaloongozwa na Mwenyekiti Ndugu Jumanne Maalam.



Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akipata maelezo ya kiwanda cha Kom Food Products co. ltd kutoka kwa msanifu wa majengo Ndugu Yusuph Daudi (kulia) wakati alipotembelea kiwanda hicho kikubwa kilichopo Kahama mkoani Shinyanga


No comments: