DC MOYO :BARABARA IRINGA RUAHA NATIONAL PARK KUJENGWA KWA LAMI MWAKA HUU

 Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiwa na baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi wakipita katika barabara ambayo inatarajiwa kujengwa kwa rami kutoka Iringa Mjini hadi hifadhi ya taifa ya Ruaha.


Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiwa na baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi wakipita katika barabara ambayo inatarajiwa kujengwa kwa rami kutoka Iringa Mjini hadi hifadhi ya taifa ya Ruaha

Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiwa na baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi wakipita katika barabara ambayo inatarajiwa kujengwa kwa rami kutoka Iringa Mjini hadi hifadhi ya taifa ya Ruaha.

Na Fredy Mgunda, Iringa.
MKUU wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo amewahakikishia watalii kuwa barabara ya Iringa hadi hifadhi ya taifa ya Ruaha itajengwa kwa lami kwa kuwa benk ya dunia imeshakubari na imeshatoa fedha za ujenzi.

Akizungumza wakati wa ziara ya kitalii ya kamati za siasa za wilaya ya Iringa vijijini na manispaa ya Iringa Moyo alisema kuwa Serikali na benk ya ipo tayari kuhakikisha mwaka huu kwa ajili ya kurahisisha usafiri kufika katika hifadhi ya taifa ya Ruaha.

Moyo alisema kuwa lengo la Serikali na benk ya dunia ni kuhakikisha wanakuza utalii wa nyanda za juu kusini kupitia hifadhi ya taifa ya Ruaha ambayo imekuwa na vivutio vingi ambayo kila mtalii anatamani kuvitembelea.

Alisema kuwa Serikali ya wilaya ya Iringa imeacha shughuli zote ambazo walizipanga kuzifanya kando kando ya barabara hiyo ili kupisha ujenzi wa barabara ambayo inamanufaa makubwa kwa wananchi wa Iringa na taifa kwa ujumla.

Moyo aliwaomba wananchi wote ambao barabara hiyo inawapitia kutoa ushirikiano kwa wakandarasi ambao watakuwa wanajenga barabara hiyo.

Alisema kuwa kukamilika kwa ujenzi wa barabara hiyo kutasaidia kukuza uchumi wa wananchi wa wilaya ya Iringa na taifa na kuleta maendeleo kutokana kuongezeka kwa watalii katika hifadhi ya taifa ya Ruaha.

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Manispaa ya Iringa Saidi Rubeya alisema kuwa kukamilika kwa ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami kutasaidia kukuza utalii kwa wananchi wa Iringa.

Rubeya alisema kuwa changamoto ya barabara hiyo kunasababisha kupunguza watalii wazawa kutokana na kushindwa kufika hifadhi ya taifa ya Ruaha kwa kutumia magari yao madogo ambayo wananchi wengi wanayo.

Alisema kuwa anapenda kuipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ya kuvitangaza vivutio vingi vya utalii vilivyopo nchini Tanzania.

Rubeya alisema kuwa ziara ya Royal Tour imeleta mafanikio makubwa na itaendelea kuleta neema kwa wananchi na taifa kwa kuongeza wawekezaji na watalii ambao watachochea maendeleo ya nchini.

Naye mwenyekiti wa wilaya ya Iringa vijijini wa chama cha mapinduzi (CCM)Costantino Kiwele alisema kuwa wanapongea hatua ya mkuu wa Wilaya kuwawezesha kutembelea hifadhi hiyo ya pili kwa ukubwa nchini, Wakiweka bayana kuanzia sasa wao ni mabalozi rasmi ya hifadhi hiyo ya taifa

Kiwele alisema kuwa baada ya kufanya utalii kwenye vivutio ya hifadhi ya Ruaha watakuwa mabalozi wa hiyari kuvitangaza vivutio vilivyopo kwenye hifadhi hiyo.

Alisema kuwa hifadhi hiyo imekuwa inamchango mkubwa kwa jamii kutokana na fedha inayoingiza kusaidia katika kutatua changamoto mbalimbali za kimaendeleo kwa wananchi.

Kiwele aliongeza kuwa hifadhi ya Ruaha imekuwa chachu ya kuutangaza mkoa wa Iringa na Tanzania kwa ujmla hivyo wanaunga mkono alichokifanya Mheshimiwa Rais kwenye Royal Tour ambayo imeanza kuleta neema kwa watanzania

No comments: