WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala bora Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa amekabidhi misaada mbalimbali yenye thamani ya zaidi ya Mil.46 kwa waathirika wa tukio la moto ulioteketeza nyumba 21 katika Kitongoji cha Shaurimoyo kijiji cha Nyamwage kata ya Mbwara Wilaya ya Rufiji Mkoani Pwani.
Mheshimiwa Mchengerwa aliwatembelea waathirika hao wa moto sanjari na kutoa saada huo ambao umepatikana kwa ushirikiano wa Kampuni ya mafuta ya Lake Oil.
Aidha Mheshimiwa Mchengerwa amekabidhi msaada huo kwa uongozi wa kitongoji ambao ni pamoja na mabati 800 yenye thamani ya Mi.22 22, mahindi tani 5 mchele tani 5 magodoro 50, mafuta lita 105 sukari kilo 210 mabalo 10 ya nguo na maharage tani 2.
Alisema sadaka hiyo ya aina mbalimbali za vyakula itawasaidia wananchi hao hadi kufikia kipindi cha msimu ujao wa mavuno.
Wakati huohuo Mheshimiwa Mchengerwa aliwataka wananchi hao kuanza maandalizi ya kilimo kwa ajili ya msimu ujao wa kilimo.
Katika misaada hiyo kati ya bati hi 800 alizokabidhi kila kaya iliyokuwa ikimiliki nyumba imegawiwa bati 30 ili waweze kujenga nyumba zao Ili maisha yaendelee na familia zao kama awali ambapo kwa sasa wamehifadhiwa kwa ndugu na jamaa zao kijijini hapo.
Aidha katika mkutano huo Mheshimiwa Mchengerwa aliwaomba wadau mbalimbali wa maendeleo kujitokeza kuchangia kwa hali na mali wananchi hao ambao kwa sasa wanaishi kwa kusaidiwa na ndugu na jamaa zao kijijini hapo.
Alisema wananchi hao wanamahitaji mbalimbali yakiwemo ya vyakula, malazi na mavazi hadi watakapoimarika na kurejea katika hali yao ya kawaida.
"Tuwaombe Wadau mbalimbali waliopo hapa Rufiji na maeneo mengine kujitokeza kusaidia wananchi hao ambao wamefikia zaidi ya 200 bado wanamhitaji mbalimbali" alisema Mheshimiwa Mchengerwa.
Mheshimiwa Mchengerwa aliongeza kwa kusema kuwa wadau hao kupeleka misaada yao kupitia Mkuu wa wilaya hiyo Meja Edward Gowele ili kupata uhakika wa misaada hiyo kuwafikia walengwa.
Aidha Mheshimiwa Mchengerwa alimeshukuru Mkuu wa wilaya hiyo kwa ushirikiano mkubwa aliotoa kwa wananchi hao ikiwa ni pamoja na kuwashukuru Wananchi na uongozi wa kijiji hicho kwa utulivu walioonesha tangu Agosri 30 mwaka huu.
WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS UTUMISHI NA UTAWALA BORA ATOA MSAADA WA MI.46 WAATHIRIKA WA MOTO RUFIJI MKOANI PWANI
Reviewed by TUPASHANE
on
September 05, 2021
Rating: 5
No comments: