TBS YAWATAKA WAHANDISI KUSHIRIKI MCHAKATO WA UANDAAJI VIWANGO
Mkaguzi wa TBS Bw. Domisiano Rutahala akitoa elimu ya masuala ya viwango kwa wateja waliotembelea banda la TBS lililopo katika maonesho ya 18 ya wahandisi yanayofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Mrisho Kikwete jijini Dodoma. TBS imetoa wito kwa wahandisi kushiriki mchakato wa uandaaji wa viwango kwa kutoa maoni ili kuleta tija kwa taifa.
Mkuu wa Maabara ya Uhandisi Ujenzi (TBS) Mhandisi William Mahona akitoa elimu kuhusu upimaji wa mabomba ya plastiki kwa wateja waliotembelea Banda la TBS lililopo katika maonesho ya 18 ya wahandisi yanayofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Mrisho kikwete jijini Dodoma.
WAHANDISI wametakiwa kushiriki mchakato wa uandaaji viwango ili kuleta ulewa wa pamoja katika viwango vya kitaifa vinavyoandaliwa kwa bidhaa mbali mbali zinazozalishwa hapa nchini, hatua ambayo itawezesha bidhaa kuwa na ubora kutokana na upatikanaji wa viwango vya kitaifa kwa wingi.
Wito huu umetolewa leo na Bw. Domisiano Rutahala, Mkaguzi (TBS), wakati wa maonesho ya 18 ya wahandishi yanayoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Mrisho Kikwete Dodoma.
Wahandisi ni semehu muhimu sana katika uzalishaji uzalishaji wa bidhaa hapa nchini hivyo basi ushiriki wao katika mchakato wa uandaaji viwango kwa kutoa maoni kutaleta tija kwa Shirika na taifa kwa ujumla. Alisema Bw. Rutahala
Pia, Bw. Rutahala alifafanua kwamba mchakato wa uandaaji viwango huusisha wadau mbali mbali katika sekta husika ambao hukutana na kuandaa viwango vya kitaifa na baadaye viwango vilivyoandaliwa huwekwa kwenye tovuti ya TBS kwa ajili ya kupata maoni na kuwaomba wahandisi kushiriki mchakato huu muhimu ili kuleta tija kwa taifa.
Aidha alitaja faida ya viwango ambazo ni kuleta usawa katika uwanja wa biashara, kurahisisha biashara baina ya nchi na nchi,na hulinda afya na usalama wa watumiaji wa bidhaa.
Kwa upande wake Afisa Masoko(TBS) Bi Rhoda Mayugu amesema maonesho haya yametumika kama sehemu ya kutoa elimu kwa umma kuhusu majukumu ya TBS ambayo ni pamoja na kuthibitisha ubora wa bidhaa, usajili wa majengo ya chakula na vipodozi, usajili wa chakula na vipodozi, na msaada wa kiufundi kwa wasafirishaji wa bidhaa nje ya nchi.
Kwa upande wa wajasiriamali wadogo na wakati TBS huthibitisha ubora wa bidhaa bure lengo likiwa ni kuhakikisha bidhaa zote zinazozalishwa hapa nchini zinakidhi ubora wa bidhaaa, hivyo basi tunatoa wito kwa wajasiriamali kuhakikisha wanatumia fursa hii.
No comments: