TANZANIA YAKIPIGIA CHAPUO KISWAHILI KUTUMIKA MIKUTANO YA UNWTO

Na Mwandishiwetu 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro awasilisha ajenda ya  kutaka lugha ya Kiswahili ianze kutumika kama lugha ya mawasiliano na lugha ya kufundishia katika mikutano  itakayokuwa ikiandaliwa  na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya utalii Duniani ( UNWTO) 

 Amesema kiswahili ni lugha inayozungumzwa na mataifa 13  na pia ina  wazungumzaji takribani milioni 150 duniani.

Kufuatia hali hiyo, Dkt.Ndumbaro alipenyeza ajenda hiyo wakati akichangia hoja za kuimarisha utalii hususan katika kuziwezesha Jamii kushiriki moja kwa moja katika shughuli za utalii katika mkutano wa 64 wa Kimataifa wa Kanda ya Afrika ulioandaliwa na  UNWTO ambao umemalizika kufanyika katika Kisiwa cha Sal nchini Cape Verde

Katika mkutano huo ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akiwa ameambatana na Waziri wa Utalii na Mambokale Zanzibar, Mhe.Lela Mussa Mohammed.

Akipenyeza ajenda hiyo ya lugha ya Kiswahili kuanza kutumika kama lugha ya kufundishia ambayo ilipokelewa,  Dkt.Ndumbaro amesema mi muda muafaka sasa kwa UNWTO kuifanya lugha ya kiswahili kama lugha ya mawasiliano kwa vile lugha nchi 13 ambao ni wanachama wa UNWTO wanazungumza lugha hiyo 

Amesema kwa kuwa lugha zinazotumiwa kwa sasa ni  Kireno, Kiingereza, Kifaransa, Kiswahili pia kitumike katika mikutano hiyo ya UNWTO kwa vile lugha hiyo imejitosheleza.

Aidha, Amesema lugha ya Kiswahili ni lugha ya tatu duniani kwa ukubwa duniani na imekuwa ikitumika kama lugha ya mawasiliano kayo katika Umoja wa nchi za Afrika ( AU ) Shirikisho la Afrika Mashariki (EAC) pamoja na nchinWanachama wa SADC

Hivyo, Dkt.Ndumbaro alishauri kuwa kwa vile mwakani Tanzania itakuwa Mwenyeji wa mkutano huo wa 65 wa Kimataifa wadau wengi wa utalii wataelewa kama lugja ya Kiswahili itatumika kama lugja ya kufundishia baadala ya kuendelea kutumia lugha ambazo ni idadi ndogo ya watu ndio wanayoimudu huku akisisitiza kuwa lugha hizo zinauhusiano wa moja kwa moja Wakoloni.

Naye Waziri wa Utalii na Mambo Kale Zanzibar Mhe.Lela Mussa Mohamed amesema licha ya ajenda ya kiswahili kupokelewa katika mkutano huo itakuwa ni ajenda ya kudumu kwa nchi zote 13 kuisemea kila wanaposhriki katika mikutano iliyoandaliwa na UNWTO kwa lengo la kukifanya Kiswahili kuwe ni miongoni mwa lugha zitakazokuwa zikitumika katika mikutano hiyo.

'' Huu ni utambulisho wetu wana Afrika Mashariki na Afrika kiujumla lazima tuhakikishe lugha ya kiswahili inatumika katika mikutano hii ili watu wetu wajue nini kinachozungumzwa kina uhusiano wa moja kwa moja kwenye maisha yao.'' alilisitiza Mhe. Lela

Kwa upande wake, Mbunge wa Kondoa mjini na Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii amepongeza uthubutu huo wa Dkt.Ndumbaro wa kuipigania lugha ya kiswahili na kusisitiza kuwa kutumika kwa lugha hiyo kitakuza utambulisho wa Tanzania na Afrika kwa ujumla 

Kufuatia hali hiyo, amishauri Serikali kuhakikisha kila fursa kama hizo zinapojitokeza hususan katika mikutano ya kimataifa ajenda ya lugha ya Kiswahili kutumika isiachwe pembeni.

Naye Mbunge wa Rorya, Mhe.Jafari Chege ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii, amesema kupenyezwa kwa ajenda ya Kiswahili ni moja ya hatua muhimu kwa vile kama lugha ya Kiswahili kitajadiliwa na kuanza kutumika katika mafunzo ambayo yataanza kutolewa na UNWTO yatachagiza maendeleo makubwa ya utalii nchini.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro ( kushoto) akizungumza na Waziri wa Utalii wa Kenya, Mhe.Najib Balala mara baada ya kumalizika kwa Mkutano  wa Kimataifa wa 64 wa Utalii Kanda ya Afrika uliomamalizika kufanyika nchini humo, Wa pili kulia ni Waziri wa Utalii nchin Cape Verde ambapo wamesema kuwa lugha ya Kiswahili iwe ni agenda ya kudumu katika mikutano hiyo ili Lugha ya kiswahili iweze kutumika kama lugha ya kufundishia na mawasiliano katika mikutano ya UNWTO.
.Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii, Zurab Pololikashvili ( wa pili kushoto)  akiwa na baadhi ya Viongozi wa Cape Verde wakiwa wamesimama mara wakiimba wimbo wa taifa wa taifa hili katika Mkutano  wa Kimataifa wa 64 wa Utalii Kanda ya Afrika uliomamalizika kufanyika nchini humo, Wa pili kulia ni Waziri wa Utalii nchin Cape Verde, Mhe. Carlos Santos
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro (katikati) akiwa na Balozi wa Paris Ufaransa Mhe.Samwel Shelukindo pamoja na Mawaziri kutoka nchi mbalimbali barani Afrika wakifuatilia mada mbali mbali za kukuza utalii wakati wa  Mkutano  wa Kimataifa wa 64 wa Utalii Kanda ya Afrikakabla ya kumalizika kufanyika katika kisiwa cha SAL nchini Cape Verde 
Baadhi ya Mawaziri wa Utalii Barani Afrika pamoja na Watalaamu wa masuala ya Utalii Duniani wakifuatilia Mkutano  wa Kimataifa wa 64 wa Utalii Kanda ya Afrika uliomamalizika kufanyika katika kisiwa cha SAL nchini Cape Verde 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro ( kushoto )  akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Utalii na Mambo Kale Zanzibar  mara baada ya kumalizika kufanyika kwa Mkutano  wa Kimataifa wa 64 wa Utalii Kanda ya Afrika  katika Kisiwa cha SAL nchini Cape Verde

No comments: