Serikali , sekta binafsi kushirikiana kuchagiza mauzo bidhaa za kilimo nje

SERIKALI ya Tanzania imesema itaendelea kushirikiana na sekta binafsi kuhakikisha kwamba taifa linaongeza mauzo ya mazao ya kilimo katika soko la kimataifa.

Imesema kwa kutanua soko hilo kutasaidia wakulima wa Tanzania kupata faida zaidi katika kilimo chao na taifa kunufaika wka pato la kigeni.

Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Profesa Siza Tumbo wakati akizindua Chumba cha Majadiliano Kilimo-Biashara 2021.

“Kila kitu tunachozalisha katika kilimo kinatakiwa mahali Fulani duniani,” alisema Profesa Tumbo katika hafla hiyo iliyoandaliwa na Taasisi Ya Mapinduzi ya Kijani barani Afrika (AGRA).

Uzinduzi huo ulihudhuriwa pia na wizara na taasisi zinazohusika katika mnyororo wa thamani kwenye kilimo, sekta binafsi Makamu wa Rais wa Agra, Vanessa Adam, Mwakilishi mkazi wa IFAD, Jacquiline Machangu na Katibu Mkuu mstaafu Wizara ya Kilimo, Peniel Lyimo aliyesimamia mjadala.

Alisema pamoja na Tanzania kujihakikishia usalama wa chakula, wakati umefika kwa sekta binafsi kushirikiana na serikali kusafirisha bidhaa nyingi za kilimo ili kuleta tija miongoni mwa wakulima na hivyo kuwawezesha kukua kiuchumi kwa wakulima wadogo .

Alisema ili kuwezesha bidhaa zaidi za wakulima kusafirishwa nje ni vyema kwa sekta ya umma, serikali na sekta binafsi kushirikiana kufungua soko zaidi soko la nje.

Profesa Tumbo alitolea mafanikio katika kilimo cha maharage aina ya soya ambapo kiliongezeka kutoka tani 3,500 mwaka 2019/2021 hadi tani 60,000 kwa mwaka 2020/2021 kutokana na juhudi za opamoja za serikali na sekta binafsi.

Naibu katibu huyo alitaka kuwepo na ushirikiano wa dhati wa sekta binafsi na umma kuhakikisha kwamba mazao yote ya wakulima yanapata soko ili kuwapatia kuipato na kuongeza kipato kwa taifa.

Chumba cha majadiliano kilimo biashara ni maandalizi ya Jukwaa la Mapinduzi ya kijani Afrika (AGRF),litakalofanyika Nairobi, Kenya kuaniza Septemba 6 mwaka huu.

Meneja Mkazi wa AGRA, Vianey Rweyendela, alisema kwamba majadiliano hayo yamelenga kuwaweka pamoja watu wa sekta binafsi , umma, serikali na wawekezaji kuona namna nzuri ya kuwawezesha wakulima wadogo kuwa na faida na kilimo chao.

Mwakilishi wa sekta binafsi, Geoffrey Kirenga, ambaye pia ni Ofisa Mtendaji MKuu wa Southern Agricultural Corridor of Tanzania (SAGCOT) alisema kufanyakazi kwa pamoja kati ya serikali,sekta binafsi nay a umma ni msingi mkubwa katika maendeleo ya kilimo na masoko nchini.


 

No comments: