MJASIRIAMALI AELEZA NAMNA FAMILIA YAKE ILIVYONUFAIKA NA UJUZI WAKE.




Na.Khadija Seif, Michuzi TV

MJASIRIAMALI visiwani Pemba amekiri kuwa ujuzi ukitumika vizuri kwa vizazi vijavyo unaweza kusaidia kupatikana kwa riziki za kila siku ndani ya familia na jamii kwa ujumla kuliko kutegemea kuajiriwa.

Akizungumza na Mkurugenzi wa Taasisi ya Warrior Women foundation Sabra Machano, Mjasiriamali wa Halua aliyefahamika kwa jina la Mohammed Saleh ambae ameamua kutumia ujuzi kwa Mke wake pamoja na watoto ili kupata pesa kwa ajili ya kukidhi Mahitaji yao ya kila siku.

"Biashara hii ya Halua nimetoa ujuzi kwa Wazee wangu na kuhamisha kwa familia yangu ninapokua nje kidogo na nyumbani najua kabisa Kuna watu ambao wanaendelea na biashara hii ya halua hivyo Sina shaka na Hilo wapo ambao nimewafundisha namna ya kupika halua."

Hata hivyo ziara ya Taasisi hiyo imekitaka kambi katika visiwa vya Pemba kwa ajili ya utafiti pamoja na kujifunza mengi kupitia wajasiriamali, nakuweza kukutana na baadhi ya wajasiriamali wakiwemo wakina Mama ambao wanatengeneza bidhaa mbalimbali za kutoa taka katika miili ambayo ni za kiasili (Singo), vungu na Mikoba.

Kupitia ukurasa wa Mtandao wa kijamii wa Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Sabra Machano amewashukuru wajasiriamali hao na kusema kuwa asili haipotei na inatumika kutafuta riziki.

"Tupo katika Mtaa wa Mandugu chakechake,tunashukuru kutupatia fursa hii kuona asili haipotei na inatumika kutafuta riziki."


 

No comments: